Introduction to Android development-Swahili
Android development ni mchakato wa
kuunda na kuboresha programu za simu za
Android. Android ni mfumo wa uendeshaji
unaotumiwa sana kwenye vifaa vya
kielectronic kama vile simu za mkononi na
vifaa vingine vya kielectronic. Programu za
Android zinaweza kuundwa na lugha
mbalimbali za programu kama vile Java au
Kotlin.
Kabla ya kuanza kujifunza Android
Development, ni muhimu kuwa na maarifa
ya msingi ya programu na uwezo wa
kusimamia lugha za programu kama vile
Java au Kotlin
Unaweza ukajifunza kila kitu kuhusiana na
lugha hizi kwenye tovuti ya
BONGOCLASS.COM.
Maarifa ya XML pia ni muhimu, kwani faili
za muundo wa programu za Android kwa
mtumiaji yaani mwonekane zake zote
zinatumia lugha hii ya XML huo.
Android Development inajumuisha
mchakato wa kubuni programu, kuandika
kanuni na kuboresha programu hiyo ili
iweze kufanya kazi vizuri kwenye vifaa
tofauti vya Android. Kuna seti ya zana na
rasilimali zinazotolewa na Google kwa
wahandisi (Developers ) wa programu za
Android kufanikisha lengo hili.
Moja ya zana zinazotumiwa sana katika
maendeleo ya Android ni Android Studio.
Ni mazingira rasmi ya development yaliyotolewa na Google ambayo hutoa
huduma za kuunda, kuandika na kujaribu
programu za Android. Android Studio
inatoa vifaa vingine vya muhimu kama vile
SDK Manager , yaani hii SDK Manager ni
Mdhibiti miundo ya ujenzi na vifaa vya
kujaribishia programu yako kama vile
emulator ya Android.
Kuna mambo kadhaa muhimu ya
kuzingatia wakati wa kufanya Android
Development, kama vile kufuata muundo
sahihi wa programu, kushughulikia
utendaji, kusimamia rasilimali, na
kuhakikisha usalama wa programu. Pia,
kuna miongozo na viwango vilivyowekwa na
Google ambavyo wahandisi (Developers) wa
programu wanapaswa kufuata ili kuunda
programu bora na salama za Android.
Kwa kumalizia, Android Development ni
mchakato wa kuunda na kuboresha
programu za simu za Android. Inahitaji
maarifa ya msingi ya programu, lugha za
compyuta(Programming Language) kama
Java au Kotlin, na maarifa ya XML. Android
Studio ni chombo muhimu kinachotumiwa
katika mchakato wa Kutengeneza Android
App, na kuna mambo kadhaa ya kuzingatia
ili kuunda programu bora na salama za Android
0 Comments