Utangulizi wa java
Kama umejifunza Java tayari endelea kujifunza software developmentJava
Ni lugha ya compyuta maarufu iliundwa mwaka 1995. Hadi sasa inamilikiwa na Oracle na inatumika ndani ya zaidi ya vifaa Billion tatu (3).
Java inatumika katika
- Programu za simu ( Hasa Android Apps)
- Programu za Kompyuta ( Desktop Application)
- Programu za wavuti (Web Application)
- Seva za Wavuti na Seva Tendaji ( Web server and Application server)
- Gemu (games)
- Muunganiko Katika Kanzidata( Database Connection)
Kwa nini java??
- Java inatumika katika platform tofauti tofauti kama vile ( Windows,Mac, Linux, Raspberry Pi, Android)
- Lugha maarufu duniani
- Ina soko kwenye ajila
- Ni rahisi kujifunza na kutumia
- Ipo Hadharani na ni Bure
- Ina usalama , ipo fasta na ina nguvu pia.
- Ina jamii ya watu wengi zaidi ya watu million 10 wanatumia hivyo ni rahisi kusaidika ukiwa na changamoto.
- Inatumia nadhalia ya vitu halisi kitu kinachofanya code na programu zieleweke, inaruhusu code kutumika zaidi ya mara moja ina punguza baadhi ya gharama.
Baada ya hayo ni wakati unaweza kuandika programu yako yenye mfano halisi katika maisha.
Hapa haikuhitaji uwe na ujuzi wowote wa programming.
Kwenye java, Application huanza na jina la class na lazima lifanane jina na ulivyo save.
Tengeneza faili ya java Main.java, itakayo fanya kazi ya ku print neno "Hello World".
public class Main{
public static void main (String [ ]args){
System.out.println("Hello World");
}
}
MAJIBU:
Hello World
Usijali ikiwa hauelewi chochote kuhusiana na code hizo hapo juu, saizi zingatia namna ya kufanya ili zilete majibu hayo.
Twende katika video ili kuhamu na kujifunza kwa vitendo tulicho andika hapa....
Tazama video hii kuelewa zaidi
.....
0 Comments