Variable (A)
variables ni container ya kuhifadhi data value ( thamani za taarifa).
Kuna aina tofauti za tofauti za variable kwenye java.
Mfano
String
Huifadhi maneno kama vile " Hello" String value huwa ndani ya double quotes
int
Huifadhi namba nzima ambayo (20) hazina decimal mfano 123 au -123
float
Huifadhi floating point number namba ambazo zina decimal mfano 19.99 au 19.99
char
Huifadhi character moja ( herufi moja) kama vile 'a' au 'B' char values huzungukwa na single quotes.
boolean
Huifadhi values zenye hali mbili tu true or false ( ndio au Hapana)
Declaration (creating) variables
Utengenezaji wa variables
Kutengeneza variable lazima utaje aina na uipe Value.
Syntax ( utaratibu wake )
type variableName =value;
ambapo type (aina) ni moja ya aina katika java kama tulivyo taja hapo awali katika java (kama vile int au String) na variableName ni jina la variable hiyo kama utakavyo amua wewe( mfano umri au rangi).
Na alama ya sawasawa (=) hutumika kuipa value , variable yako.
Ili kutengeneza variable ambayo ita hifadhi maneno tazama mfano huu.
Mfano
Tengeneza variable iite rangi aina ya String ipe value yake **njano**
String rangi = "njano";
System.out.println(rangi);
Ili kutengeneza variable ambayo ita hifadhi namba tazama mfano huu.
Mfano:
int umri = 15;
System.out.println(umri);
Vile vile unaweza ku tangaza uwepo wa variable flani kwenye programu yako bila kuipa thamani (value) na ukaipa thamani (value) baadaye.
Mfano.
int kiasi;
kiasi = 1000;
System.out.println(kiasi);
Zingatia
Kama utaipa value mpya variable ambayo tayari ina value, compila itaenda kutambua variable mpya na sio ile ya zamani.
Mfano:
int umri =15;
umri = 20; // sasa umri ni 20
System.out.println(umri);
Final variables
Kama hauhitaji kubandika value mpya java language imeandaa neno ambalo ukilitumia compaila ina elewa una maanisha ya kuwa hautaki kubandika value kwenye variable yenye value tayari na neno hilo ni **final** kwenye java hijulikana kama moja ya keyword.
Aina zingine
int umri = 5;
float mgao = 5.33f;
char herufi = 'D';
boolean hali = true;
String neno = "Habari";
**Print variable ( B) **
Ku display variable ( ku print variable)
println() method hutumika ku display variable
Kuunganisha maneno na variable alama ya (+) hutumika.
Mfano
String jina="John";
System.out.println("Habari " +jina);
Output: Habari John
Vilevile unaweza kutumia (+) kuunganisha variable moja na ingine.
Mfano
String jinalakwanza = " John ";
String jinalapili = "Jiku ";
String jinakamili = jinalakwanza + jinalapili;
System.out.println(jinakamili)
Output: John Jiku
Kwa value ambazo ni namba (+) hufanya kazi kama alama ya kujumlisha katika hesabu ( kumbuka tunavyo shughulika na namba tuna tumia aina ya data ambayo ni int)
Mfano
int ada = 100;
int nauli = 200;
System.out.println (ada + nauli);
Output: 300
Kutoka katika mfano hapo juu unaweza ukaelewa
-ada imehifadhi thamani ya 100
-nauli imehifadhi thamani ya 200
- kisha tunatumia println() method ku display thamani ( value) ya ada + nauli ambayo ni 300.
Mwisho wa Somo 5
Jiunge na group la Telegram HAPA kujifunza zaidi.
Tazama video YouTube video masomo yote HAPA
0 Comments