Java tutorial somo la 13
Methods
hii ni block ya code ambayo huwa inarun muda ambao inahitajika
unaweza pitisha taarifa (data) maarufu kama parameters , kwenye method
method inatumika kufanya jambo flani na pia huitwa functions
kwa nini method zinatumika, hii ni ili kutumia code zaidi ya mara moja kwa kuzitengeneza mara moja tu
create method ( tengeneza method )
method lazima iwe declared ndani ya class , inakuwa defined na jina la method yenyewe ikifuatiwa na mabano ya
namna hii ().
java programming language ina method zake nyingi tu mfano
System.out.println();
lakini pia unaweza tengeneza method kwa ajili ya kufanya takwa lako flani
mfano:
public class Main{
static void myMethod(){
// block ya code zako hapa
}
}
Maelezo ya mfano huo hapo juu
- myMethod ni jina la method
- static hii ina maana kuwa method inamilikiwa ndani ya Main class na sio kama sifa ya Main class
Utajifunza zaidi kuhusu objects na jinsi ya kutaja methods kwenye objects
- void hii ina maaana kuwa method haina return value yoyote.
utajifunza zaidi kuhusu return value muda sio mwingi
Call Method( kutaja method)
kutaja method kwenye java, andika jina la method ikifuatia na mabano ya namna hii ()
na kisha semicolon ( ; )
kwenye mfano myMethod imetumika ku print maneno ( shuguli) pindi inapo tajwa .
mfano
Ndani ya main , taja myMethod() method
public class Main {
static void myMethod (){
System.out.println(" nafurahi kukumbukwa");
}
public static void main ( String [] args){
myMethod();
}
}
output: nafurahi kukumbukwa
vilevile method inaweza tajwa zaidi ya mara moja na ikafanya ivyo ivyo.
public class Main {
static void myMethod(){
System.out.println("nimefurahi kukumbukwa !" );
}
public static void main ( String [] args){
myMethod();
myMethod();
myMethod();
}
}
output: nimefurahi kukumbukwa !
nimefurahi kukumbukwa !
nimefurahi kukumbukwa !
Parameters and Arguments
- Taarifa zinaweza kupitishwa kwenye method kama parameters
- Parameters zinakuwa kama vile variables ndani ya methods
- parameters hutajwa baada ya jina la method ndani ya mabano ()
- unaweza kuwa na parameters nyingi kwa kadri unavyotaka wewe kwa kuzitenganisha na comma (,)
mfano ufuatao unamethod inayo chukua String inaitwa fname kama parameter pindi method inapotajwa.
tunapitisha jina la kwanza kwenye method ambayo ndani ya method itatumika ku print jina kamili
mfano
public class Main {
static void myMethod( String fname){
System.out.println( fname + " Tech " );
}
public static void main (String []args)
{
myMethod("Jiku ");
myMethod("Eden");
myMethod(" Basanzie");
myMethod( " Tanzania");
}
Output: Jiku Tech
Eden Tech
Basanzie Tech
Tanzania Tech
ZINGATIA:
parameter inapitishwa kwenye method huitwa argument. Hivyo kutoka kwenye mfano
fname ni parameter ambapo Jiku, Eden, Basanzie na Tanzania ni arguments
Multiple Parameters
unaweza kuwa na parameters nyingi kwa kadiri unvyo weza na kupenda wewe.
mfano
public class Main {
String fname ,int age){
System.out.println ( fname + " ana miaka " + age);
}
public static void main (String [] args ){
myMethod("Jiku " , 27);
myMethod("Eden " , 31);
myMethod("Basanzie " , 28);
myMethod("Tanzania " , 62);
}
}
output: Jiku ana miaka 27
Eden ana miaka 31
Basanzie ana miaka 28
Tanzania ana miaka 62
Java Return Value
Kwenye maelezo yaliyopita tulitumia void keyword kwenye mifano yote ambayo humaanisha method haitakiwi ku return
value yoyote.
kama unataka method yako i return value, unaweza kutumia moja kati ya primitive data type kama vile int ,char , n.k
badala ya void na tumia return keyword ndani ya method yako.
mfano
public class Main{
static int myMethod(int x) {
return 5+ x;
}
public static void main ( String [] args) {
System.out.println( myMethod (3));
}
}
output: 8 ( kwa sababu 5 + 3 ni 8)
vilevile unaweza kuhifadhi majibu kwenye variable ( inapendekezwa kwa sababu ya urahisi wa kusoma na kudhibiti)
mfano
public class Main {
static int myMethod(int x , int y ) {
return x+y;
}
public static void main ( String []args) {
int z = myMethod(5,3);
System.out.println(2);
}
}
Output: 8
Java Scope
Method Scope
variable zikiwa declared moja kwa moja ndani ya method basi zinaweza tumika popote ndani ya method
mfano
public class Main {
public static void main(String []args){
//code zote hapa hazi wezi kutumia x
int x = 100;
// code za hapa zinaweza kutumia x
System.out.println(x);
}
}
Block Scope
block ya code ni code zote ndani ya mabano ya namna hii {}
variable ikiwa declared ndani ya block ya code inatumika na code katika mabano ya aina hii {}
kuanzia ilipo kushuka chini
mfano
public class Main{
public static void main (String [] args ){
//code za hapa hazi tambui x
{ // hii ni block ya code
// code za hapa hazi tambui x
int x = 100;
// code za hapa zinawza kutumia x
System.out.println(x);
} // block inaishia hapa
//block ya code za hapa haziwezi tumia x
}
}
Mwisho wa Somo la 13;
0 Comments