Privacy Policy

Header Ads Widget

Java Syntax SOMO 2

 Somo 2

Java syntax




Kwenye somo lililopita tulitengeneza faili ya java Main.java na tulitumia code hapo chini ku print " Hello World".

public class Main{

public static void main( String [ ] args) {

System.out.println("Hello World");
}
}

Maelezo ya mfano huu ni kama ifuatavyo.

Kila mstari wa code unao run kwenye java huwa ni lazima uwe ndani ya class.  Kwenye mfano wetu tumeita class Main na class mara zote lazima ianze na Herufi kubwa ya kwanza.

Zingatia Java ni
case-sensitive: MyClass na myclass ni vitu vyenye maana tofauti  katika java.

Vilevile jina la file la java ni lazima lifanane nanjina la class . Wakati una save faili i save kwa kutumia jina la class na ongezea ".java" mwishoni mwa jina la faili yako.

Ili ku run izo code hapo juu lazima uhakikishe una mazingira kama maelezo kwenye video iliyopita na majibu lazima yaje.

Hello World


Uwepo wa main Method
main() method inahitajika mara zote na utaiona karibia kila programu.

Hii
public static void main( String [ ] args ); code zote ambazo zipo ndani ya main() method zita kuwa executed. Na usiwaze kuhusu maneno hayo kabla na baada ya main utaenda kuya elewa kidogo kidogo unavyo endelea kusoma hii kozi.

Kwa sasa , jitahidi sana kukumbuka kuwa kila programu ya java ina jina la class ambalo lina kuwa linafanana na jina la file na kila programu inakuwa na main() method ndani yake.


System.out.println( )
Ndani ya main() method, inaweza ikatumika println() method ku print mstari au mistari ya maneno kwenye screen Yako.
Kama ilivyo "Hello World"

public static void main ( String [ ]args){
System.out.println("Hello World");
}

ZINGATIA

- curly braces {} ni alama ya kutambulisha mwanzo na mwisho wa block ya code .
- System yenyewe ni class ya java ambayo imeundwa ndani ya lugha ya java nayo ina wahusika wake kama "out", ambaye ni kifupisho cha "output" .  println() method ni kifupisho cha neno " print line " .
Inatumika ku print value kwenye screen ( au file)

- Usijali sana kuhusu System, out na println(). Tambua tu kwamba unazihitaji kwa pamoja ili ku print kitu kwenye screen.

- Ni muhimu kutambua kwamba kila sentensi ya code lazima iishie na semicolon (;).

JIPIME

Zoezi

Chukua karatasi na peni ujaze sehemu zilizo achwa wazi kwa ajili ya ku print "Hello World".

public class MyClass{
public static void main (String [ ]args){

_________ . _______ . _______("Hello World");
}
}

Mwisho wa Somo la Leo la Java Syntax.


Katika somo lijalo tutasoma JAVA OUTPUT 

Post a Comment

0 Comments