BROWSER AU KIVINJALI KATIKA MATUMIZI YA MTANDAO
Jifunze jinsi ya kuwa mahili katika matumizi ya mtandao
Karibu tena katika makala hii ambayo nitaenda kukufahamisha kipengele muhimu katika umahili wa kutumia mtandao
Imekuwa ni mazoea kwa watu wengi hata mimi kujihusisha katika jambo moja kwa moja wakilenfa kupata pesa katika jambo hilo kitu kinacho pelekea kama una mtu anakutegemea basi wewe siku ambayo hauja pata pesa anakuwa na wakati mgumu sana.
Nimezungumza hiyo kauli kwa sababu ya ukweli kwamba ukisoma kipengele hiki kidogo hautapata pesa kwahiyo ni kama ladhi kwako ndugu msomaji.
Mtu akiumia katika mpira wale watoa huduma ya kwanza wanakuwaga na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kukamilisha suala la huduma ya kwanza. Kama umewahi kupika basi wewe ni shahidi kwamba ili ukamilishe kupika lazima upite katika vipengele vingi ndio ukamilishe suala zima la kupika.
Leo katika kujifunza namna ya kuwa bora katika matumizi ya internet tuta jifunza na kuzungumza kwa kifupi kuhusiana na kivinjali, ili uwe bora katika matumizi ya internet basi lazima ufahamu vipengele vingi kuhusian na internet.
Mtu alie gundua internet aliwapa watu wengine fursa ya kujipatia kipato. Kwani ili uweze kuifikia internet katika mambo mengi lazima utumie kivinjali chochote.
Kivinjali au browser ni program ya computer ambayo inakusaidi wewe kufikia wavuti mbalimbali kwenye mtandao mfano wa wavuti ni kama www.mpandamc.go.tz na mfano wa kivinjali au
browser ni
Google chrome
Fire fox
Opera Mini
[ Je una taka kujifunza zaidi kuhusiana na PROGRAM ZA COMPUTER ??
Ili kufahamu kuhusiana na program za computer mtu inakubidi upate muda kidogo tu kujisomea kuhusiana na mafunzo ya computer kwa ujumla wake
Unaweza ukasoma makala yangu kufahamu hayo <<ufahamu wa computer>> au unaweza gharamia kitabu changu cha ufahamu wa computer kwa gharama ya TZS 5000/= kwa mawasiliano zaidi 0682 329 852
]
Nahitimisha kwa kusema ili ufanikiwe katika kuwa mahili wa kutafuta taarifa mtandaoni au kujifunza chochote mtandaoni ni lazima uelewe kuwa borwser au kivinjali kwa kiswahili ndio kama njia ya wewe kuingilia tovuti yoyote ile duniani.
Mwingine anajua na mwingine hajui, sasa kwa yule ambaye hajui mchakato upo hivi ukitaka kuingia mtandaoni lazima cha kwanza uwe na bando la internet kwenye simu yako na uwashe data katika simu yako hatua ya pili utafuta kivinjali kwenye simu yako au komputa yako ambayo ndio njia ya kuingilia mtandaoni, kisha baada ya hapo utakutana na ingini ya utafutaji ambayo inakuwa ime setiwa na wewe au automatic kama ingini ya utafutaji kuu kwenye browser yako
Tutajifunza kuhusiana na ingini ya utafutaji katika makala ingine usiache kutembelea blog yangu mara kwa mara.
0 Comments