UTANGULIZI KUHUSIANA NA COMPUTER
Nini maana ya computer
Kompyuta ni kifaa cha kielektroniki ambacho huchukua taarifa/maagizo kutoka kwa mtumiaji na kuchakata taarifa / maagizo hayo chini ya udhibiti wa mipangilio ya maelezo maalum (inayoitwa programu) na kutoa matokeo (pato) na kutunza matokeo hayo kwa matumizi ya siku zijazo. Inaweza kuchakata hesabu za nambari na zisizo za nambari (hesabu na kimantiki).
Mwanzoni kabisa ilikuwa ikijulikana kwamba mtu anae fanya mahesabu makubwa na kwa ufanisi basi ndio walimwita computer lakini kwa sasa hivi computer imekuwa ni kifaa kinacho tumia umeme kinacho fanya kazi automatic kwa kuongozwa na mtumiaji kwa namna anayo itaka yeye
History of Computer
Historia ya Computer
Kabla ya yote kwenye ufahamu wako tambua kwamba computer ni kama neno Computing ambalo linashabiiana na neno calculating na pia neno calculating ni sawa na kurahisisha yaani simplifying
Computer —>>> Computing
Computing —-->>>>Calculating== calculator
Calculating →>> Simplifying
Hayo ni mambo ambayo mtu unatakiwa kufahamu katika kichwa pindi unapo skia neno computer
Tuendelee,,,,, Watu wa zamani walitumia vijiti, mawe na muda mwingine mifupa kufanya mahesabu yao na hivyo vilikuwa kama vifaa vya kuhesabia
Lakini maendeleo ya ubongo wa mwanadamu na Kukua kwa technology kuliendelea na kupelekea kuwepo kwa mapinduzi mbalimbali.
Muda ulivyo zidi vifaa vingine vilikuwa vikigunduliwa
Katika ugunduzi wa computer devices
Kuna vizazi vingi ambavyo ni kama mabolesho matano yaliyo fanyika kutoka ugunduzi hadi sasa
Hadi sasa tupo kwenye generation ya tano ambayo ina
Desktop Computer
Laptop Computer
NoteBook
UtlaBook
ChromeBook
Importance of computer skills
Katika kipindi hiki cha kidigitali, Ujuzi wa computer umekuwa ni muhimu sana ili kufanikiwa katika majukumu yaliyopo katika maeneo mbalimbali maishani. Maeneo hayo hususani kielimu, kazini na mambo binafsi
Computer na vifaa mbalimbali vya umeme vimeleta mapinduzi ya namna tunavyo takiwa kuishi , namna tunavyo weza kufanya kazi, namna tunavyoweza kutafuta taarifa , namna tunavyo weza kuwasiliana na wengine na namna tunavyo weza kufanikisha shughuli zetu kiurahisi na kwa ufanisi mkubwa
Hizi ni baadhi ya sababu za kwa nini ujuzi wa komputer ni muhimu katika kipindi hiki cha kidijitali ??
UFANISI: Kwa kutumia computer unaweza fanya kazi kwa haraka na kwa ufanisi (yaani haraka na bila kukosea) kwa mfano unaweza tumia computer kuandaa nyaraka , kutuma barua pepe na kufanya utafuta wa taarifa za kitafiti mbalimbali kwa njia ya mtandao (online search) huu ujuzi utakusaidia kurahisha utendaji na kuongeza uwezo wako kwa kuokoa muda
MAWASILIANO: computer na vifaa vya kidijitali vimerahisisha namna ya kufanya mawasiliano kwa urahisi. Kwa kutumia ujuzi wa computer unaweza wasiliana na mtu kupitia Email, mikutano ya video ,Mitandao ya kijamii, na majukwa mbalimbali ya mtandaoni duniani kote.
MAENDELEO YA KAZI: Fursa mbalimbali za kazi siku hizi zinahitaji sana kuajili mtendaji ambaye angalau anakuwa na ujuzi wa computer. Kwa kuwa ujuzi wa computer unampa mtu uwezo wa kutumia Program mbalimbali za computer, Uwezo wa kufanya utafiti na Na ujuzi au uwezo wa kupangilia taarifa mbalimbali na kuzichakata kwa ufanisi. Kwa hivyo katika kipengele hiki uwezo mzuri wa kutumia computer unaweza kukutofautisha na wengine katika fursa flani .
UTAFUTAJI WA TAARIFA: Ujuzi wa computer una mpa mtu uwezo wa kutafuta taarifa rasmi mbalimbali rasmi katika mtandao. ( Internet) kwa kutumia search engine ( engine za utafutaji) mtu unaweza tafuta taarifa yoyote kuhusiana na jambo lolote mtandaoni mahali popote pale duniani.
UBUNIFU: Kwa kutumia ujuzi wa computer mtu anaweza fanya jambo lolote la kibunifu kwa kutumia computer yake kwa namna anavyo taka. Mfano mtu anaweza fanya uzalishaji wa video anaweza tengeneza mitindo mbalimbali ya kibunifu ( graphics designing) , uzalishaji wa muziki.
AINA ZA UJUZI WA COMPUTER
ujuzi wa komputa kwa upana unaweza kusemwa kwa namna mbili
Moja ujuzi wa kimsingi
Pili Ujuzi wa kitaalamu
Ujuzi wa kimsingi
Ujuzi huu anahitaji mtu yoyote anaye taka kutumia computer kwa matumizi madogo madogo kama vile kutuma barua pepe , kutumia mitandao ya kijamii, utafutaji wa taarifa mtandaoni na kukamilisha taarifa mbalimbali za kiofisi.
Huu ni baadhi ya ujuzi muhimu katika ujuzi wa kimsingi wa computer
Kuendesha Mifumo endeshi ya computer kwa ufanisi mfano Windows na MacOs kwa maana ya kufungua na kufunga program mbalimbali , Kutengeneza na Kutunza Files pamoja na Kurekebisha mipangilio mbalimbali ya computer
Kutumia Program za kuchakata documents/nyaraka kama vide program ya Microsoft Office ambayo hutumika kuandaa nyaraka mbalimbali kama vile maandiko ya ofisini, barua, na repoti
Kutumia ujumbe wa kinelectronic emails ,mtu ataweza kutuma na kufungua email zinazo ingia katika kifaa chake. Ataweza kutuma files na viambatanisho vya picha,video,docs nk
Kuvijari kwa kutumia vivinjali kama vile Google Chrome na Firefox Mozilla ambazo hutumika kufungua internet katika kifaa kwa ajili ya kutafuta taarifa mtandaoni kupitia wavuti na kujaza fomu mbalimbali mtandaoni.
Kutumia Mitandao ya kijamii, kama vile Facebook, Twitter, LinkedIn katika kufanya mahusiano (networking), Masoko na Mawasiliano.
Ujuzi wa kitaalam/ Ujuzi wa hali ya juu
Huu ni ujuzi/taaluma maalamu ambao ni kwa ajili ya jambo maalam na ujuzi wenyewe unahusisha maarifa ya juu ya software program, Lugha mbalimbali za computer na mifumo mbalimbali ya computer yaan complex computer systems
Hapa ni mifano ya ujuzi wa juu wa computer
Programming: hii ina husisha kunadika code kwa kutumia lugha za computer kama vile Java, C, C++, Python nk ujuzi wa juu katika kipengele hiki no pamoja na utengenezaji wa Complex Algorithm na Application mbalimbali,. Unaweza ukawa hauelewi kinacho zungumziwa hapa kwa sasa ila kwa mbele utapata picha kamili..
Web Development Hii ni taaluma ya kutengeneza wavuti mbalimbali kama unavyo ona www.bongoclass.com hii ni tovuti ya kitanzania inayo jihusisha na elimu katika masuala mbalimbali ya kijamii na kitechnolojia.
Graphics design
Data analysis
AINA ZA COMPYUTA
Aina za kompyuta zinaweza kuelezewa kwa namna mbili kulingana na ukubwa pamoja na uwezo wa kuchakata taarifa kama ifuatavyo
AINA ZA KOMPYUTA KULINGANA NA UCHAKATAJI WA DATA
1. Analogue Computer
2. Digital Computer
3. Hybrid Computer
Analogue Computer
Hizi ni kompyuta ambazo utendaji kazi wake ni wa moja kwa moja yaani inavokuwa inachukua data ni zinatumika zilizo ivo ivo amna kuchakatwa tofauti na aina zingine za computer ambazo taarifa lazima zibadilishwe kuwa binary data na kisha kuchakatwa mfano wa computer hizi ni Speedometers na Mercury Thermometer
Digital Computer
Hizi ni computer ambazo zimeundwa mahususi kwa ajili ya ku-perform calculation na logical operation kwa speed ya hali ya juu. Yenyewe inachukua taarifa kwa mfumo wa binary yaa 0 na 1 na kuzichakata kwa kutumia programu ambazo zinakuwa zimehifadhiwa ndani ya computer
Mfano wa komputer hizi ni zile zote za kisasa kama vile laptops na desktop computer pamoja na simu janja ( smartphone)
Hybrid Computer
Hizi ni kompyuta ambazo zina namna kama analogue na digital computer yaani zina Speed kama analogue computer na zina ufanisi kama digital computer kompyuta hizi mara nyingi zina tumika hospitalini , kwenye ndege na kwenye maswala mazito ya utafiti wa kisayansi.
Jinsi ya kupata pesa mtandaoni
Jinsi ya kutengeneza email
Jinsi ya kuingia kwenye email yako ya zamani
Blogging na pesa mtandaoni soma kwa makini
Mafunzo ya computer kwa kiswahili
Aina za computer
Nini maana ya database
AINA ZA KOMPYUTA KULINGANA NA UKUBWA
1. Supercomputer
2. Mainframe computer
3. Mini Computer
4. Workstation computer
5. Personal Computer
Supercomputer
Hii ni aina ya computer ambayo imeundwa kwa namna ya kuchakata ma trillion ya taarifa kwa sekunde moja tu kompyuta kama hizi mara nyingi zinakuwepo ofisi za hali ya hewa kwa ajili ya utabili wa hali ya hewa . Zingatia hii computer inaweza kuchakata ma trillion ya taarifa kwa sekunde moja tu.
Utengenezaji wa siraha za nyukilia unategemea computer ya aina hii, masoko ya hisa yanategemea computer hizi ungozaji wa satellite unategemea computer hizi
Mainframe computer
Hii ni computer ambayo imeundwa kwa uwezo wa kutumiwa na ma elfu ya watu kwa wakati mmoja , kompyuta hii inauwezo wa ku run maelfu ya program tendaji kwa wakati mmoja na kwa ufanisi na mantiki hii ndio inawezesha utendaji rafiki kwenye mashirika ya Bank na Mitandao ya Simu Telecom organization Ndani ya bank inarecord ma million ya miamala kwa wakati mmoja , ndani ya Telecom Org ina wezesha mamillion ya miunganiko ya mawasiliano kwa wakati mmoja.
Minicomputer
Hii ni aina ya kompyuta ambayo ni kama mdogo wa mainframe ambayo yenyewe inakuwa na uwezo wa kutumiwa na watu kuanzia wa nne hadi mia mbili ( 4-200) kwa wakati mmoja na mara nyingi hutumika kwenye mataasisi na department kwa ajili ya masuala ya fedha na mahesabu ya fedha hii ni computer ambayo inakuwa na uwezo na ukubwa ambao ni kati ya mainframe na microcomputer
Workstation computer
Hii ni computer yenye uwezo wa kutumiwa na mtu mmoja, microprocessor yake inakuwa na speed kubwa pia inakuwa na RAM kubwa na mara nyingi computer hizi huundwa kwa ajili ya kazi flani maalum mfano graphics workstation, music workstation au engineering workstation
Personal Computer/microcomputer
Hii ni computer ambayo imeundwa kwa namna ya kuwa na matumizi mengi na ni kwa ajili ya matumizi ya mtu mmoja mmoja. Laptops na Desktop computer zote kwa pamoja ni microcomputer.
Hadi hapa mjadala wa aina za computer unakuwa umeisha, kwa mujibu wa andiko hili lakini pia kuna mahala unaweza kuwa hauja elewa jambo ambalo sio la kuwa na wasiwasi kabisa kwa maana safari bado inaendelea ya kujifunza computer kwa undani kuna maneno yameandikwa yanaweza kukuchanganya lakini usijali mda sio mwingi utakuwa na ufahamu nayo.
Pia baada ya kujifunza matumizi ya mtandao katika kurasa zijazo utakuwa na uwezo wa kufuatilia jambo lolote kwa undani kwa kutumia kivinjali na injini ya utafutaji
Ufahamu kuhusina na Software na Hardware (computer systems)
Unapo zungumzia komputa kuachana na tafsri yake halisi ina mifumo miwili mifumo ambayo ni software na hardware mifumo ambayo inawezesha utendaji kwa ufanisi
Vifaa vyote vya kushikika kwenye computer (phisical componets) huitwa Hardware
Mkusanyiko wa programs tendaji mbalimbali zinazo toa amri jinsi gani hardware ifanye kazi kwa kufuata maelekezo maalum huitwa Software
Programu/Software
Seti ya maagizo ambayo huambia vifaa vya kompyuta(Hardware) nini cha kufanya inajulikana kama programu za kompyuta. Programu hii au mkusanyiko wa programu kama hizo hujulikana kama programu za kompyuta. Dhana ya programu imeonyeshwa kwenye takwimu ifuatayo:
Kiufupi katika computer software ni kama akili bandia softwares hutoa maelekezo kulingana na utaratibu au utendaji ulio kusudiwa na mtengenezaji wa hiyo software kwa ajili ya kutatua matatizo au tatizo flani katika ulimwengu au jambo lake binafsi
Aina za software
Kwenye computer software zipo za aina mbili ambazo ni
Software Endeshi (System Software )
Software Tendaji (Application Software)
Software tendaji huwa na zana mbalimbali kwa ajili ya utendaji rafiki kwa mtumiaji kulingana na kazi anayo ifanya
Mfano wa Software tendaji ni kama
Microsoft excel
Microsoft word
PowerPoint
Google chrome
Virtual dj studio
Games
Software Endeshi hii ni mifumo endeshi ya computer ambapo ili computer ifanye kazi lazima iwe na mfumo endeshi mfano wa mfumo endeshi wa computer ni kama
Microsoft Windows
Linux
Mac n.k
Mifumo hii imeundwa ili kuwezesha utendaji fanisi kwa mifumo tendaji {software application} software tendaji inafanya kazi kwenye computer yoyote au kwenye kifaa chochote kutegemeana na uwepo wa software endedhi katika kifaa hicho
Mfumo endeshi pia kazi yake kubwa huwa ni kufanya muunganiko wa vifaa vya hardware kwenye komputa na kuendesha au kuwezesha ufanyaji kazi wa software zingine kwenye computer
UTENDAJI KAZI WA COMPUTER KWA UFUPI
Computer ilivumbuliwa kutona na vifaa vidogovidogo (chukulia mfano vifaa vidogo vya watoto vinavyo wasaidia katika somo la hesabu shule za msingi - vihesabio) hadi sasa karne ya 21 ya computer zilizo kamilika katika utendaji mbalimbali kwa karne chache tu tangu kuvumbuliwa hadi sasa.
Pamoja na kuwepo kwa technology ya kisasa hivi sasa, ni wazi kwamba watu wengi hawaelewi ni kwa jinsi gani kipande kama cha ubao mnene kidogo (computer) kina uwezo wote wa kufanya mahesabu magumu hadi kuja kuliza muziki, kucheza video na kuendesha mifumo mingine.
Unapo sema utendaji kazi wa komputa, ili uelewe fikilia namna ubongo wa binadamu unavyo fanya kazi katika changamoto mbalimbali, ila sasa kwa computa ni fasta zaidi yaani ufanyaji kazi ni ule ule japo kuna utofauti
Komputa inafanya kazi kwa speedi, bila kukosea na bila kuchoka yenyewe chakula chake ni umeme tu .
Ubongo wa binadamu unafanya maamuzi taratibu taratibu sana , unaweza kukosea na unachoka. Huu ndio utofauti mama kati ya ubongo na computer.
Juu ya yote hayo, computer hufanya kazi kwa hatua nne tu hadi kutoa majibu ya mchakato husika, yaani unavyo bonyeza batani yako kwamba iandike namba tisa, inapitia hatua nne ndio unaiona namba tisa, iwe ni kwenye simu, calculator au kifaa chochote kama unavyo kumbuka tafsri au maana ya computer.
Hatua nne za utendaji kazi wa computer
Input: Input is the data before processing. It comes from the mouse, keyboard, microphone, and other external sensors.
Storage: The storage is how the computer retains input data. The hard drive is used for long-term and mass data storage while the data set for immediate processing is stored temporarily in the Random Access Memory (RAM).
Processing: Processing is where input gets transformed into output. The computer's Central Processing Unit (CPU) is its brain. It's responsible for executing instructions and performing mathematical operations on the input data.
Output: Output is the final result of data processing. It can be anything from images, video, or audio content, even the words you type using a keyboard. You can also receive the output through a printer or a projector instead of directly through your device.
1. MAINGIZO: Hizi ni taarifa kabla ya mchakato mfano wa hizi ni zile zinazotoka kwenye keyboard, kipanya, maiki, na vifaa vingine vya namna hii
2. KUMBUKUMBU: Kwa hapa kumbukumbu tunayo izungumzia ni kwa namna gani komputa inahifadhi taarifa zake. Nna imani unafahamu kama simu inakuwaga na memory ya ndani ifananishe na Hard Disk Drive kwenye computer memory hizi hutumika kuhifadhi taarifa kwa muda mrefu lakini kwa taarifa ambazo zina tumika muda huo huo hukaa kwenye aina nyigine ya memory ndani ya computer ambayo inaitwa Random Access Memory RAM memory hii huhifadhi taarifa za mchakato unao endelea.
3. MCHAKATO: Hapa ndipo taarifa hubadilishwa na akili ya komputa na kutoa majibu. Kichakato kikuu cha komputa (KIKU) ndio akili ya computer (Central Processing Unit-CPU)
Hii majukumu yake ni kuchakata taarifa kwa kufuata maelekezo maalum yanayo iwezesha kufanya mahesabu makubwa ili kutoa majibu yanayo tarajiwa na mtumiaji
4. MAJIBU: haya ni matokeo ya mwisho baada ya uchakataji wa taarifa ambapo yanaweza kuwa picha, video, audio/sauti na hata maneno unayo kuwa unachapa kwenye keyboard yako
Vifaa vya computer kwa ndani
MATUMIZI YA COMPUTER KULINGANA NA MFUMO ENDESHI NA SURA YA MTUMIAJI
Utangulizi
Mfumo endeshi katika computer huwa kama kiunganishi kati ya computer hardware na mtumiaji wa computer . Lengo la mfumo endeshi haswa huwa ni kuwezesha mazingira kwa mtumiaji katika kufanikisha uchakataji wa taarifa kwenye program za computer
Maana ya mfumo endeshi
Mfumo endeshi ni programu ambapo husimamia ufanyaji kazi wa application program (
Maana ya mfumo endeshi
Hii ni program maalum ambayo inasimamia utendaji kazi wa program tendaji zote kwenye kompyuta na kuwa kama uwanja au mazingira unganishi kati ya vifaa vya hardware na programu za software mbalimbali pamoja na mtumiaji wa komputa
Mfumo endeshi katika komputa ni kama serikali ambayo inafuata mfumo wa ujamaa ambao maamuzi mengi yanafanyika na serikali na hivyo serikali inakuwa mpangaliaji na mgawaji wa rasilimali za nchi.
Hivyo hivyo katika computer mfumo endeshi wa computer hufanya kazi ya kugawa rasilimali hitajika kwa kila program kwa muda mmoja. Mfano halisi ni vile kwenye computer unaweza cheza video mbili kwa wakati mmoja sababu ya mazingira wezeshi yanayo wezesha namna hiyo mazingira rafiki yanayo toka kwenye aina husika ya mfumo endeshi
Na hapo kwenye kucheza video mbili kumbuka spika inayotumika inakuwa moja kompyuta na zinaskika sauti ya video zote mbili, hivyo basi Operating Systems huwezesha mazingira kwa mtumiaji kufanikisha matakwa yake kwa kutumia program tendaji zilizomo ndani ya computer.
MAJUKUMU YA MUHIMU YA MFUMO ENDESHI KATIKA KOMPUTA
KURATIBU RASILIMALI: mahitaji sambamba au ya pamoja ya rasilimali kwenye kompyuta yakitokea basi mfumo endeshi wa komputa unakuwa ni mratibu katika suala hili , kutokana na uhitaji wa rasilimali husika.
KURATIBU MICHAKATO INAYO ENDELEA: kwa kutumia kifaa kigumu au hardware componet inayoitwa CPU kwa kiswahili KIKU mfumo endeshi hupangilia michakato yote inayo endelea kwa ajili ya kifaa (computer) kufanya kazi kwa ufanisi ueredi ulio pangilika.
KURATIBU UHIFADHI : Mfumo endeshi kwa kutumia taratibu maalum kama vile NIFs, CFs, CIFs, NFs ( kwa uelewa wa vifupisho hivi unaweza kutumia mtandao wa google kujua ufafanuzi wake), kwa namna mbalimbali mfumo endeshi huratibu upangaji , utambuzi na uhifadhi wa taarifa katika computer.
KURATIBU KUMBUKUMBU: mfumo endeshi kwa kutumia taratibu maalum kama vile ni kumbukumbu za kiasi gani zimetumika na zimetumika na nani katika komputa , inafanya maamuzi na maandalio ya kiasi gani cha memory inayo hitajika kulingana na mchakato husika.
KURATIBU SUALA LA ULINZI NA USALAMA : Mfumo endeshi huundwa na namna yake ya kusimamia suala la salama yaani passwords na mamlaka flani katika utumizi wa mifumo au mfumo tendaji flani. Mfano mfumo endeshi wa kampuni ya Microsoft , Windows Os hutumia kanuni zinazoitwa Kerberes katika kusimamia usalama na kutoa mamlaka.
Ili komputa iweze kuendesha program zingine ni lazima ndani yake iwe na mfumo endeshi wa kutekeleza suala hilo mfumo endeshi huwezesha matumizi ya hardware na mifumo endeshi mingine kwa watumiaji wengine
Mfumo endeshi ni muunganiko wa program maalum zinazo fanya kazi kwenye komputa ili kuwezesha utendaji sahihi na fanisi wa komputa.
Aina za mifumo endeshi ya computer
Batch Operating System
Hii ni aina ya mfumo endeshi wa komputa ambao ukisha washwa tu hautegemei mwingiliano tena na mtumiaji, mfumo huu unafanya kazi kama taa ambayo huwashwa ili kutoa mwanga tu na kuzimwa mahitaji yanavyo isha bila mwingiliano wowote na mtumiaji wa aidha kupunguza au kuongeza mwanga, hivyo hivyo mfumo huu ukiwashwa hufanya kazi iliyo wajibu wake na kuzimwa .
Time sharing Operating System
Hii ni aina ya mfumo endeshi ambayo kazi yake kubwa ni mwingiliano wa rasilimali kwenye komputa zaidi ya moja.
Distributed Operating System
Hii ni mfumo endeshi ambao unawezesha uwezo wa kuongoza komputa nyingi na zifanye kama komputa moja.
Network Operating System
Huu ni mfumo ambao ni maalum kwenye computa iliyo undwa kukubali mifumo endeshi ya aina mbalimbali.
Real time Operating System.
Sifa za mfumo endeshi wowote
Uwe na uwezo wa karatibu kumbukumbu
Uwe na uwezo wa kuratibu michakato
Uwe na uwezo wa kuratibu mfumo wa files
Uwe na uwezo wa kuratibu vifaa shikika na laini katika matumizi yake
Uwe na uwezo wa kuratibu suala la usalama kwa namna pendwa
Uwe na namna ya mazingira rafiki kwa mtumiaji ( sura ya mtumiaji) interface kwa kiingereza kwa ajili ya kutumia na kufanya shughuli mbalimbali.
Uwe na uwezo wa kufanya na kuratibu miunganiko ya aina mbalimbali (Networking)
MIFUMO ENDESHI MAARUFU DUNIANI
Microsoft Windows
Apple macOs
Google’s Android OS
Apple iOS
Linux Os
Microsoft Windows
Huu mfumo unakuwepo tangu 1980 na inamatoleo na mabolesho kama vile Windows 95, Windows Vista , Windows 7/8/10 na hadi sasa mwaka 2023 Windows 11.
Huu ni mfumo endeshi pendwa duniani kote na watumiaji wa mfumo huu pendwa wanapendelea sababu ikiwa ni unawezeshe na ni rafiki kwa matumizi ya software mbalimbali bila shida
Mfumo huu endeshi unamilikiwa na kampuni kubwa ya microsoft inc
Apple macOs
Huu ni mfumo endeshi maarufu ambao kibiashara una ushindani mkubwa na kampuni ya Microsoft Inc , watumiaji wa mfumo huu wanasema mfumo huu ni rahisi kuutumia unafanya kazi kwa speed ni smooth ( laini ) na pia unawezesha kuunganisha simu janja na komputa
Google Android OS
Huu ni mfumo endeshi zaidi ni maarufu kwenye simu janja
Apple OS
Huu pia ni mfumo endeshi kwa ajili ya simu
Linux OS
Huu ni mfumo endeshi ambao upotofauti na mifumo mingine ni mfumo ambao unaruhusu kuufanyia marekebisho yoyote kwa mujibu wa mtumiaji .
Licha ya mifumo hii mitano maarufu duniani pia kuna nyingine nyingi sana za mifumo endeshi duniani.
UFAHAMU KUHUSIANA NA SURA YA MTUMIAJI YA MFUMO ENDESHI
(GRAPHICAL USER INTERFACE)
GUI
Ni njia ya kuwasiliana nini unachotaka kwenye programu ya computer kwa kutumia graphical symbols badala ya kutumia maelezo mengi kwenye GUI unaweza kubofya picha mishale ili kuendelea au kufungua kitu flani kulingana na alama iliyopo.
GUI ina utajili wa alama kuliko maelezo, alama ambazo zina msaidia mtumiaji kufanya miondoka ya namna mbalimbali na hivyo ili kuwa mahili katika sura ya mtumiaji ya mfumo wowote ni lazima ujifunze au upate uzoefu wa alama hizo.
VIPENGELE KATIKA GUI VINAVYO MWEZESHA MTUMIAJI WA KUINGILIANA NA PROGRAMU ZA KOMPYUTA KWA URAHISI
Button: A graphical representation of a button that acts as a program when pressed.
Dialogue box: A type of window that displays additional information and asks a user for input.
Icon: Small graphical representation of a program, features, or file.
Menu: List of commands or choices offered to the user through the menu bar.
Ribbon: Replacement for the file menu and toolbar that groups programs activities together.
Tab: Clickable area at the top of a window that shows another page or area.
Toolbar: Row of buttons, often near the top of an application window, that controls software functions.
Window: Rectangular section of the computer's display that shows the program currently being used.
0 Comments