Privacy Policy

Header Ads Widget

Aina za Computer

 

Aina za Computer











Aina za kompyuta zinaweza kuelezewa kwa namna mbili kulingana na ukubwa pamoja na uwezo wa kuchakata taarifa kama ifuatavyo 


AINA ZA KOMPYUTA KULINGANA NA UCHAKATAJI WA DATA


1. Analogue Computer

2. Digital Computer

3. Hybrid Computer


Analogue Computer





Hizi ni kompyuta ambazo utendaji kazi wake ni wa moja kwa moja yaani inavokuwa inachukua data ni zinatumika zilizo ivo ivo amna kuchakatwa tofauti na aina zingine za computer ambazo taarifa lazima zibadilishwe kuwa binary data na kisha kuchakatwa mfano wa computer hizi ni Speedometers na Mercury Thermometer


Digital Computer


Hizi ni computer ambazo zimeundwa mahususi kwa ajili ya ku-perform calculation na logical operation kwa speed ya hali ya juu. Yenyewe inachukua taarifa kwa mfumo wa binary yaa 0 na 1 na kuzichakata kwa kutumia programu ambazo zinakuwa zimehifadhiwa ndani ya computer 

Mfano wa komputer hizi ni zile zote za kisasa kama vile laptops na desktop computer pamoja na simu janja ( smartphone)


Hybrid Computer


Hizi ni kompyuta ambazo zina namna kama analogue na digital computer yaani zina Speed kama analogue computer na zina ufanisi kama digital computer kompyuta hizi mara nyingi zina tumika hospitalini , kwenye ndege na kwenye maswala mazito ya utafiti wa kisayansi.


Mada Zinginezo


AINA ZA KOMPYUTA KULINGANA NA UKUBWA

1. Supercomputer

2. Mainframe computer

3. Mini Computer 

4.  Workstation computer

5. Personal Computer


Supercomputer


Hii ni aina ya computer ambayo imeundwa kwa namna ya kuchakata ma trillion ya taarifa kwa sekunde moja tu kompyuta kama hizi mara nyingi zinakuwepo ofisi za hali ya hewa kwa ajili ya utabili wa hali ya hewa . Zingatia hii computer inaweza kuchakata ma trillion ya taarifa kwa sekunde moja tu.

Utengenezaji wa siraha za nyukilia unategemea computer ya aina hii, masoko ya hisa yanategemea computer hizi  ungozaji wa satellite unategemea computer hizi 


Mainframe computer


Hii ni computer ambayo imeundwa kwa uwezo wa kutumiwa na ma elfu ya watu kwa wakati mmoja , kompyuta hii inauwezo wa ku run maelfu ya program tendaji kwa wakati mmoja na kwa ufanisi na mantiki hii ndio inawezesha utendaji rafiki kwenye mashirika ya Bank na Mitandao ya Simu Telecom organization Ndani ya bank inarecord ma million ya miamala kwa wakati mmoja , ndani ya Telecom Org ina wezesha mamillion ya miunganiko ya mawasiliano kwa wakati mmoja.


Minicomputer


Hii ni aina ya kompyuta ambayo ni kama mdogo wa mainframe ambayo yenyewe inakuwa na uwezo wa kutumiwa na watu kuanzia wa nne hadi mia mbili ( 4-200) kwa wakati mmoja na mara nyingi hutumika kwenye mataasisi na department kwa ajili ya masuala ya fedha na mahesabu ya fedha    hii ni computer ambayo inakuwa na uwezo na ukubwa ambao ni kati ya mainframe na microcomputer 



Workstation computer


Hii ni computer yenye uwezo wa kutumiwa na mtu mmoja, microprocessor yake inakuwa na speed kubwa pia inakuwa na RAM kubwa na mara nyingi computer hizi huundwa kwa ajili ya kazi flani maalum mfano graphics workstation, music workstation au engineering workstation 




Personal Computer/microcomputer


Hii ni computer ambayo imeundwa kwa namna ya kuwa na matumizi mengi na ni kwa ajili ya matumizi ya mtu mmoja mmoja. Laptops na Desktop computer zote kwa pamoja ni microcomputer.


Hadi hapa mjadala wa aina za computer unakuwa umeisha, kwa mujibu wa andiko hili lakini pia kuna mahala unaweza kuwa hauja elewa jambo ambalo sio la kuwa na wasiwasi kabisa kwa maana safari bado inaendelea ya kujifunza computer kwa undani kuna maneno yameandikwa yanaweza kukuchanganya lakini usijali mda sio mwingi utakuwa na ufahamu nayo.

Pia baada ya kujifunza matumizi ya mtandao katika kurasa zijazo utakuwa na uwezo wa kufuatilia jambo lolote kwa undani kwa kutumia kivinjali na injini ya utafutaji


Post a Comment

0 Comments