Hatua 6 za Kubobea lugha flani ya compyuta
Hatua 6 za Kubobea lugha flani ya compyutaSiko mbali sana kwenye maana hii nimejitahidi kusema nilichokusudia
Jifunze java programming language hatua kwa hatua
Computer is any electrical device that take input, process it and give out an output under certain special INSTRUCTIONS and store output for future use.
INSTRUCTIONS kwenye maana ya computer ndio hapo ipo programming, yaani mchakato wa kutengeneza INSTRUCTIONS za kutumiwa na computer.
Jifunze java programming language hatua kwa hatua
Kuwa huru kuuliza swali lolote kuhusu programming ili kukuza ufahamu wako kuhusu programming kwa mtu yoyote aliye tayari kukusikiliza.
Mara mtu anapo hitaji kujifunza programming awe mwanafunzi au mtu yoyote swali huwa linakuja atajifunzaje na itawezekanaje yeye kubobea??
Watu hasa wanfunzi huangaika sana na hili kupata jinsi sahihi ya wao kujifunza programming language ( programming language maanayake lugha ya kompyuta) na wengine kuishia kujihangaisha kutamani kujifunza kwa ugumu ndani ya muda mfupi yaani fasta fasta kama wanavyokuwa wanazania wao kitu kinacho sababisha wabaki kuzunguka zunguka katika utangulizi au ujuzi wa awali bila wenyewe kujua.
Jifunze java programming language hatua kwa hatua
Wengine wanajaribu kuruka hatua na kujaribu kujifunza hatua za mbele moja kwa moja lakini inakuwa haina msaada wowote na mwisho wa siku ni muhimu kufuata mfululizo wa hatua zinazotakiwa kuweza ujuzi wa programming kwa urahisi.
Kiukweli, Kuelekea kujifunza na kubobea programming language ni rahisi na inachukua hatua kadhaa za msingi lakini tatizo ni kwamba wengi hupuuzia jambo hili kitu kinacho tengeneza ugumu kwa upande wao.
Tuangalie hatua unazotakiwa kufuata ili kujifunza na kubobea programming language.
- Fanya uchaguzi wa lugha ya kompyuta kulingana na mahitaji yako.
- Elewa na tengeneza misingi yako kuhusiana na hiyo lugha uliochagua.
- Hama kutoka ujuzi wa awali kwenda ujuzi wa juu.
- Fanya mazoezi tena,tena na tena.
- Tengeneza projects ndogo na kubwa
- Shiriki code zako na ujuzi wako kwa watu wengine.
Sasa Tuangalie hatua hizi kwa undani zaidi
Fanya uchaguzi wa lugha ya compyuta kulingana na mhitaji yako.
Kitu cha kwanza na chenye kipaumbele unatakiwa kuchagua lugha ya kompyuta kulingana na mahitaji yako kwa sababu kuna mamia ya lugha hizi za kompyuta kama vile Python, C, C++,Java, JavaScript, PHP ,Ruby na nyingine zaidi . Kwa mfano kama ukitaka kujifunza programming ikwa ajili ya kutengeneza tovuti (web development ) unaweza kuchagua lugha kama JavaScript, PHP, n k, kama unataka kujifunza lugha kwa ajili ya teknolojia inayo trendi kama vile AI na ML (Machine Language) unaweza kuchagua Python na nyingine zake.
Elewa na tengeneza misingi yako kuhusiana na hiyo lugha ulio ichagua.
Hapa ni muda wako wa kuelewa mambo yote ya awali ambayo ni muhimu kama vile sifa zake , matumizi yake, syntax zake,data type, variables n.k Hii inaweza kuchukuliwa kama mchakato wa muhimu sana kwa sababu utakutengenezea msingi wa kuelewa undani wa safari nzima ya kujifunza programming, Hata elimu zetu nyingine zinafundisha kuwa kitu cha kwanza ni kufahamu msingi kisha kuendelea mbele mfano kutoka alfabeti hadi kutengeneza aya .
Unaweza kutumia vyanzo vingi vya kujifunza vinavyo pendekezwa kama vitabu, YouTube videos, blogu kwa ajili ya kutengeneza msingi imara
Jifunze java programming language hatua kwa hatua
Hama kutoka ujuzi wa awali kwenda ujuzi wa juu.
Huu ni wakati sahihi wa kuchimba zaidi na kuingia hatua inayofuata ya ujuzi wa juu.
Unatakiwa kufahamu kwa undani nadhalia zote ndani ya programming kama vile Pointers, Dynamic Memory Allocation, File Management na Preprocessors kwenye lugha y C au nadhalia ya OOPs , Interface na Packages , Multi threading n.k kwenye JAVA.
Vile vile unatakiwa kupitia kuhusiana na Data Structure mfano Linked List, Stack,Queue, Heap n.k na Algorithms kwenye hatua hii ili kuwa bora zaidi. Kuna platform mbalimbali zipo kwenye mtandao kama vile GeekforGeeks, Javatpoint n.k ambako unaweza kujifunza mada hizi kwa upana zaidi.
Fanya mazoezi tena,tena na tena.
Kama ulivyo msemo” mazoezi huimarisha kufanya kwa usahihi”,,,,,, “Practice makes a man perfect “. Unatakiwa kufanya mazoezi kwa kiwango cha juu kwa kadiri unavyo weza ili kuimarisha ujuzi wako wa lugha ya kompyuta.
Ukiwa mzuri katika hili utapata ujasiri. Kuna namna nyingi za kuimarisha ujuzi huu kama codding challenges.
Tengeneza projects ndogo hadi kubwa.
Wakati tayari umetumia muda wako mwingi katika kufanya mazoezi ni muda sasa wa kusghulika na utengenezaji wa projects halisi.
Kutengeneza project zako mwenyewe ni jambo litakalo kufanya kubobea programming, vilevile unaweza ukachagua kuunda project ndogo na kubwa kwa kadiri unavyo jiskia na unavyo hitaji mwenyewe.
Mbinu bora ya kuunda project ya kuvutia na kibunifu kitu cha kwanza ni kufikiria kwanza tatizo au issue ambayo inaweza kutatulika kidijitali.
Hatua zifuatazo za kutatua tatizo au za kutengeneza project zinaweza kuwa msaada.
- Tambua tatizo
- Elewa tatizo
- Orodhesha suluhisho zinazo wezekana
- Chambua suluhisho hizo kwa makini
- Chagua suluhisho ambayo imekuwa bora
- Tengenezea suluhisho mtindo kwa mpangilio
- Andaa algorithm
- Andaa utekelezaji wake
- Andika programu kuu
- Kagua programu katika vipengele mbalimbali
- Kagua na ondoa errors zote
- Hitimisha.
Shiriki Code na Ujuzi wako kwa watu wengine .
Nimuhimu kushiriki na wengine kama ilivyo ujuzi sikuzote unaongezeka kadiri unavyo shiriki,,,,,, Wakati ukitaka kumfundisha mtu hakikisha umeandaa somo lililopo na atakalo elewa kupitia wewe .
Imeandaliwa na JIKU TECH TIPS
Phone 0682329852
Tukutane katika makala ingine.
Jifunze java programming language hatua kwa hatua
Facebook Jiku Jiku
Google Search: Jiku Tech Tips
Jifunze Zaidi
0 Comments