Privacy Policy

Header Ads Widget

Java Tutorial SOMO 10

 Java Tutorial SOMO 10







Java ** if  else**


Java conditions and if statements 

Java ina ruhusu kutumia logical condition za kawaida za kwenye Hesabu.



Kama vile 


 - Less than a<b

 - Less than au equal to a<=b

 - Greater than a>b

 - Greater than au equal to a>=b

 - Equal to a==b

- Not Equal to a !=b


Unaweza kutumia hizi logical condition kufanya vitu mbalimbali kutokana na maamuzi flani kwenye program yako.


Java ina condition statements zifuatazo


 - inatumika ** if ** ku specify block flani code ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi kama specified condition ni kweli.


 - Inatumika **else** ku specify block ya code ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi kama condition ya kwanza sio kweli


 - Inatumika **else if ** ku specify condition mpya ambayo ita angaliwa ikiwa Condition ya kwanza sio kweli


 - Inatumika ** switch** ku specify block mbadala za code ambazo zina takiwa kufanyiwa kazi.


**If Statement**


Tumia ** if ** statement ku specify block ya code za java zinazotakiwa kufanyiwa kazi kama condition ni kweli


**Syntax**

if ( condition) {

// block ya code kama condition ni kweli

}


Zingatia , ikitokea umeandika if kwa herufi kubwa (IF) compailer ita run error 


Tutazame mfano wa if statement 


Mfano

if (20>18){

System.out.println(" 20 ni kubwa kwa 18")

Output: 20 ni kubwa kwa 18


Tujaribishe Variables 


int x = 20;

int y = 18;

if ( x>y){

System.out.println(" x ni kubwa kwa y");


Maelezo ya mfano


Kwenye mfano hapo juu tumetumia variable **x**  na ** y** ku jaribisha kama x ni kubwa kwa y kwa kutumia Operator (>)


Kama ilivyo x ni 20 na y ni 18 , na tunajua kuwa 20 ni kubwa kwa 18, hivyo tume print  maneno ili kuthibitisha hilo kuwa ni kweli ( x ni kubwa kwa y)




else statement 


Tumia **else** ku specify block ya code ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi ikiwa condition sio kweli 


Syntax 

if ( condition) {

//block ya code ambayo inatakiwa kuwa. 

// executed ( kufanyiwa kazi) ikiwa 

// condition ni kweli


} else {

// block ya code kama condition ya hapo

// juu sio kweli

}


Mfano 

int time = 20 ;

if ( time <18) {

System.out.println("Siku njema");

} else {

System.out.println(" jioni njema");

}

Output: Jioni njema


   **else if statement**

Tumia ** else if ** statement ku specify condition mpya ikiwa condition ya kwanza sio kweli 


Syntax

if (condition1){

//block ya code kama condition1 ni kweli

}else if (condition2){

// block ya code kama condition1 ni sio

// kweli

} else {

// block ya code kama condition1 na

 // condition2 sio  kweli

}


Mfano 


int time = 22;

if ( time<10) {

System.out.println(" Habari ya asubuhi");

} else if (time <20){

System.out.println(" Habari ya mchana");

} else {

System.out.println(" Habari ya jioni");

}


Output: jioni njema


Maelezo ya mfano 

Kwenye mfano hapo juu time (22) ni kubwa kwa 10, kwa hiyo condition1 ni sio kweli


Condition inayofuata kwenye **else if ** statement na  ni sio kweli, tunaenda moja kwa moja kwenye chaguo linalo fuata ambalo ni ** else ** condition kwa vile ** condition1**  na ** condition2**  zote ni sio kweli na tuna print " jioni njema" 


Ingekuwa time =14 basi program yetu Inge print "" Habari ya Mchana ""


 **Java Switch Statement**


Tumia **switch** statement kuchagua block ya code unayotaka ifanyiwe kazo ( iwe executed) kutoka kwenye block za code nyingi


 **Syntax**

switch ( expression) {

case x:

// code block hapa

break;

case y: 

// code block hapa

break;

default:

//code block 

}

Na hivi ndivyo inavyo fanya kazi


- **Switch**  expression inakuwa evaluated kwanza

- Thamani ( value) ya expression inafananishwa na values za kila **case**

- kama ipo inayofanana basi code block kwenye hiyo case inakuwa executed ( yaani inafanyiwa kazi)


- break na default keyword ni za ziada hapa tutazijadili hapo mbele 


Mfano hapo chini umetumia namba za siku za wiki ku kukokotoa jina la siku husika.


Mfano:

int day = 4;

switch ( day) { 

case 1:

System.out.println( " jumatatu");

break;

case 2:

System.out.println( " jumanne");

break;

case 3:

System.out.println( " jumatano");

break;

case 4:

System.out.println( " alhamisi");

break;

case 5:

System.out.println( " ijumaa");

break;

case 6:

System.out.println( " jumamosi");

break;

case 7:

System.out.println( " jumapili");

break;

}


Output: Alhamisi( day 4 ) ambayo ndio siku  ya nne.


**break keyword**


Tulinena kwamba tujadili hii

java program ikifikia ** break** keyword ina achana na case zingine


Ikipata inayofanana  switch expression basi kazi ina kuwa imekamilika, na hapa ndio kuna kazi ya  keyword ya **break**

Kwani hata kama case zipo 100 ikipata inayofanana kwenye case ya 5 basi zote 96 zinazobaki zina puuzwa .



default keyword 


** default** keyword ina specify code zinazo takiwa kufanyiwa kazi ikiwa amna case inayo fanana na expression yako


Mfano 

int day = 4;

switch ( day) {

case 6:

System.out.println( " leo jumamosi");

break;

case 7:

System.out.println( " leo jumapili");

break;

default:

System.out.println("nilikuwa natazama kama siku ya nne unaitwaje na sasa nimekosa");


Mwisho wa somo la 10 

video kwenye YouTube ya Jiku Tech Tips kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.


Jifunze Zaidi

SOMO LA UTANGULIZI

SOMO LA 1

SOMO LA 2

SOMO LA 3

SOMO LA 4

SOMO LA 5

SOMO LA 6

SOMO LA 7

SOMO LA 8

SOMO LA 9

SOMO LA 10

SOMO LA 11

SOMO LA 12

SOMO LA 13




Post a Comment

0 Comments