Endelea kujifunza....
Java Math
Java math ina methods nyingi sana zinazo ruhusu kufanya kazi mbalimbali za mahesabu kwenye namba.
Math.max(x,y)
Hii ni method inatumika kutafuta thamani kubwa kati ya x na y , au kati ya namba zozote zikiwa kama hapo juu.
Mfano
Math.max(5,10);
System.out.println(Math.max(5,10));
Output: 10
Jibu ni 10 kwa sababu ndio namba kubwa kati ya (5,10).
Math.min(x,y)
Hii ni method inatumika kutafuta thamani ndogo kabisa kati ya namba x na y.
Mfano
Math.min(5,10);
System.out.println(Math.min(5,10));
Output: 5
Jibu ni 5 kwa sababu ndio namba ndogo kati ya (5,10).
Math sqrt(x)
Hii method inatumika kutafuta kipeuo cha namba .
Mfano
Math.sqrt(64)
System.out.println( Math sqrt(64));
Output: 8.0
Kwa sababu 64 kipeuo chake ni 8
Kwa kuhitimisha naweza sema uelewa mzuri ni ule wa kujua na kuelewa matumizi ya kitu.
Kwenye mfumo wa elimu ili usone taaluma hii wanataka uwe na ufaulu wa masomo ya hesabu. Kama ulivyo oona mwenyewe hapa matumizi yake , ila. Sio issue sana.
Unaweza ukajifunza zaidi kipengele hiki cha java math kutokana na mahitaji yako wakati una fanya development.
Java Boolean
Mara kibao kwenye programming utahitaji data type ambayo ina value mbili tu.
i.e
- YES/NO
- ON/OFF
- TRUE/ FALSE
Kwa hili , pia java ina data type boolean ambayo inachukua values true au false
Boolean Value
Aina ya boolean hutumika na keyword ya**boolean** na inaweza kuchukua value mbili tu true au false
Mfano
boolean javaninzuri = true;
boolean sukarinichungu = false;
System.out.println(javaninzuri);
System.out.println(sukarinichungu);
Output: true
Output: false
Vile vile ni kawaida ku return boolean values kutoka kwenye boolean expression, kwa condition testing
Boolean Expression
Hii ni java expression ambayo majibu yake ni Boolean value true au false
Unaweza kutumia comparison operator mfano kubwa kuliko ** greater than** (>) kutafuta au kuangalia kama expression au ( variable) ni kweli ( true)
Mfano
int x = 10;
int y = 9;
System.out.println(x>y);
Output: true
Kwa sababu ni kweli 10 ni kubwa kuliko 9.
Kwenye mfano unaofuata tumetumia equal to ( ==) ambayo ni operator tulijigunza kwenye somo lililolita itatumika ku evaluate expression
Mfano
int x = 10;
System.out.println( x==10);
Output: true
Kwa sababu ni kweli x = 10;
Hii ndio ** Boolean** unaweza jifunza zaidi kwenye vyanzo vingine kwa muongozo huu kuhusu boolean.
Mwisho wa SOMO 9 ,,
SOMO H
ILI LITAKUWA NA VIDEO YA KUJIFUNZA KWA VITENDO KWENYE YOUTUBE YA. ** JIKU TECH TIPS**
0 Comments