Java Operators SOMO 7
Operators kwenye java hutumika ku perform operation mbalimbali za variables na value.
Kama huelewi nini maana ya variables rejea kwenye SOMO 5 linalo eleza kuhusu variables.
Kama inavyo onekana katika mfano hapo chini alama ya kujumlisha ambayo ni moja ya OPERATOR (+) imetumika ku jumlisha value mbili.
Mfano:
int x = 100 +50;
Output 150
Hata kama (+) imetumika kumjumlisha value kama inavyo onekana kwenye mfano
Uliopita, vile vile inaweza jumlisha variable na value au variable na variable
Mfano
int sum1= 100+50; // 150 (100+50)
int sum2 = sum1 + 250;//400(150+250)
int sum3 = sum2 + sum2;// 800(400+400)
Kwenye java operators zinagawanyika kwenye makundi yafuatayo.
Arithmetic operators
Assignment Operators
Comparison Operators
Logical operators
Bitwise operators
Arithmetic Operators
Hutumika hasa kushughulika na hesabu za kawaida
Hizi ndio arithmetic operators
Kujumlisha (+)
Kujumlisha value mbili (x+y)
Kutoa (-)
Kutoa value moja kutoka kwenye nyingine
(x-y)
Kuzidisha(x)
Kuzidisha value (x*y)
Kugawanya (/)
Kugawanya value moja na nyingine(x/y)
Modulus (%)
Kuonesha namba inayo baki baada ya kugawanya namba (x%y)
Increment (++)
Kuongeza 1 kwenye value ya variable
Decrement (kupunguza )(- -)
Kupunguza 1 kwenye value ya variable
Java assignment operators
Assignment operators hutumika ku thaminisha thamani kwenye kitu ( variable)
Kwenye mfano hapo chini tumetumia alama (=) kuthaminisha thamani (10) kwenye kitu kinachoitwa (x)
Mfano
int x= 10 ;
Orodha ya assignment operators
=, +=, -=,*=,/=,%= na nyingine nyingi zaidi
Java Comparison
Hizi hutumika kulinganisha thamani mbili au vitu ( variable) . Na hii ni muhimu sana katika programming kwani husaidia kutafuta au kupata majibu na kisha code zako zika fanya maamuzi, Return value ya comparison ni kweli ( true) au sio kweli (false) .
Hizi hujulikana kama Boolean.
Tutajifunza zaidi kuhusiana na boolean na if...else mbeleni
Kwenye mfano unaofuata tuta tumia alama ya great than ( kubwa kuliko) ( >) kutafuta au kuangalia kama 5 ni kubwa kuliko 3
Mfano
int x = 5 ;
int y = 3;
System.out.println( x>y);
Output: true
Kwa sababu ni true 5 ni kubwa kwa 3
Hizi ndio alama za comparison
==
!=
>
<
>=
<=
Java logical operators
&&
Jina: Logical
Maelezo: Return true kama statement zote ni kweli
||
Jina : logical or
Maelezo: Return true kama statement moja ni kweli
!
Jina: Logical not
Maelezo: ina Reverse majibu , hii ina return false ikiwa majibu ni kweli (true)
Mwisho wa SOMO LA 7
SOMO.hili litakuwa na video
ya kujifunza kwa vitendo itapatikana kwenye YouTube channel ya Jiku Tech Tips
Subscribe kujifunza kwa vitendo.
Tazama Video ya Somo hili HAPA
Contact me: 0682329852
0 Comments