Strings kwenye java hutumika kuhifadhi au kushikilia thamani ambazo ni maneno yaani (text)
Kitu ( variable) ambacho ni ** String** hujuisha mkusanyiko wa herufi ambazo zinazungukwa na alama za funga semi na fungua semi ( quotes)
Mfano
Tengeneza kitu ( variable) ambayo ni aina ya String kipe thamani yake .
String salam = "Habari";
Kwenye java String ni Object ambayo imetengenezwa pamoja na java na ina methods zake ambazo zinaweza kufanya operation mbalimbali kwenye String
**HINT**
Method
Tunapo sema object chukulia mfano mtu ni object, tunapo sema object ina method chukulia kama vile mtu ana viungo vya kufanya kazi mbalimbali mfano kwa mtu mkono - kushika, mdomo- kutamka, miguu - kutembea n.k
Kwa mfano kwenye java ukitaka kufahamu urefu wa String yako unaweza kutumia method ( length)
Mfano
String maneno = "abcdefghijklmnopqrstuvwxyz";
System.out.println("urefu wa maneno ni : " + maneno.length() );
Kwahiyo baada ya kutambua kuwa String kwenye java ni Object na ina method unaweza jifunza zaidi ama katika Google yako ( kama hujui kutumia google ingia kwenye YouTube yangu kuna video ya mafunzo ya kutumia search engine)
Jifunze Method zote zilizomo ndani ya String object na namna ya kuzitumia na ikiwa utashindwa kusitumia ama kuzielewa ni vyema utauliza ama mimi au Google au mtu mwingine.
String Concatenation
Nadharia ya kuunganisha String kwa namna mbalimbali
Alama (+) inaweza ikatumika katika String kuziunganisha yaani kuunganisha String moja na ingne na hiki kitendo ndio kinaitwa ** String Concatenation**
Mfano
String jinalakwanza = " Jiku";
String jinalamwisho = " Tech Tips";
System.out.ptintln( jinalakwanza + " " + jinalamwisho);
** Output** Jiku Tech Tips
HINT
Tumeweka (" ") ili kuweka nafasi ya kutenganisha maneno.
- kama nilivyo kueleza String object ina method nyingi na kwenye
Mfano hapo juu:
Unaweza kutumia mbadala kuunganisha String kama ifuatavyo.
String jinalakwanza = " Jiku";
String jinalamwisho = " Tech Tips ";
System.out.println( jinalakwanza.concat(jinalamwisho));
Katika java ukisha weka namna hiyo basi compiler inaelewa kwamba ni kuunganisha String mbili.
Java Numbers na Strings
ONYO:
Lugha ya java hutumia alama ya (+) kujumlisha na kuunganisha.
Ambapo
Namba hujumlishwa na String ( text) huunganishwa .
Kama utajumlisha namba mbili majibu yatakuwa namba
int x = 10;
int y = 20;
int z = x+y;
z itakuwa 30;
Kama uta unganisha String mbili jibu litakuwa muunganiko wa String
Mfano:
String x = "10";
String y = "20";
String z = x+ y ;
Jibu la z litakuwa 1020
Kama uta jumlisha namba na string jibu litakuwa ni muunganiko wa String
Mfano
String x = " 10" ;
int y = 20;
String z = x+y;
Jibu ni 1020
JIFUNZE KWA VITENDO SOMO LA 8 TAZAMA VIDEO HII
Mwisho wa SOMO 8
Hii ndio namba kwa ajili ya mawasiliano yangu 0682329852
Somo lijalo ni HESABU kwenye java.
0 Comments