NDOTO ZA KUWA MTU FLANI KWENYE TEHAMA
NDOTO ZA KUWA MTU FLANI KWENYE TEHAMA
Kirefu Cha neno Hilo ni Teknolojia ya habari na mawasiliano, taaluma AMBAYO Hadi mwaka huu 2024 hazija waingia watu wengi na waliyo nayo wengi nchini Tanzania ni wa binafsi wa maarifa na wenye kukatisha tamaa wale wanao taka kujifunza.
Na hii ni sifa mojawapo ya baadhi ya watu waliofanikiwa kusoma TEHAMA kwenye mfumo rasmi wa nchi kuamini au kusema kujifunza taaluma hii ni kugumu na hakuna manufaa makubwa kwenye Tanzania
Kuelewa jambo lolote mara nyingi inategemea sana mapokeo ya mtu kwenye jambo hilo, kutoka Kwa yule unaye amini kuwa anaweza kukuelewesha jambo hilo, pia inategemea mazingira ya mapokeo hayo yaani kati ya mwalimu na mwanafunzi kwenye Hilo jambo.
Ufahamu wa kompyuta Kwa matumizi ya kawaida
Ikutokea unajifunza jambo flani kutoka Kwa mwalimu aliyepo hapo Kwa muda huo katikati ya watu basi namna chanya yenye kiwango Cha kuelewa jambo hilo Kwa upande wako utatokana na nguvu yako ya kupambana na mkumbo yaani Ile Hali inayojengwa na watu wakati huo kuhusu jambo hilo.
Nguvu ya kupambana na mkumbo ni pale mtu anajiongeza na kuandika pembeni nukuu kadhaa kutoka kwa mwalimu wakati huo, na siokuishia kunukuu tu mtu huyu anatafuta vyanzo vingine kwamba vinasemaje kuhusu hili jambo. Na hapo hapo mtu anapima kati ya elimu ya jambo kutoka vyanzo vingi na uwezo wake wa kipekee wa kutafakari alio pewa na mwenyezi mungu ana ng’amua Kwa kadiri yake usahihi wa jambo hilo.
Ufahamu wa kompyuta Kwa matumizi ya kawaida
Ni kweli tunajuvunia kuja Kwa elimu lakini Mimi nazani tukubali kwamba kuelewa uvumbuzi wa jambo na athari zake mbalimbali kwenye jamii ndio ukomavu wa kwamba sasa jambo nimelielewa.
Tambua kwamba asili yetu katika kuelimishana ni binafsi sana hata ukifuatilia kauli za waelimishaji wengi wa mambo mbalimbali hazijaelekeza sana kumfumbua mtu na badala yake kumfunga mtu.
Ufahamu wa kompyuta Kwa matumizi ya kawaida
Unakuta mtu mfano Mimi nimekupa mamlaka ya kunielimisha jambo flani ambalo una elimu nalo ya kiwango flani hata kama haukulianzisha, wewe ukachukua nafasi au fursa ya Mimi kutokufahamu ukaniambia Kwa namna unayoitaka yaani badala ya kunifumbua elimu ya Hilo jambo naipata wapi na misingi yake ya kujifunza ni ipi unaishia kuniambia Kwa uhakika kwamba jambo hili lipo hivi, na ukiwa hivi basi ni uongo, kitu ambacho Mimi nitakalili maneno yako na kuishi nayo na kama nisipo pata chanzonl kingine Cha kunielewesha basi nakufa na kiwango hicho hicho nilicho jifunza kwako.
Katika ukufunzi wangu wa masuala ya kidijitali nimekutana na mwanafunzi mmoja mhitimu wa kidato Cha sita kmwaka 2024 kwenye mchepuo wa PCM akinieleza kwamba yeye anapenda masuala ya Development ya Mifumo mbalimbali kupitia programming lakini ana hofu kubwa Kwa sababu mwalimu wake wa tuition alimwambia programming ni taaluma ngumu sana na hata ukisoma haina kazi kwenye Tanzania yetu Kwa kuwa jamii ya Tanzania haipo aware ( haina uelewa) kuhusu masuala hayo.
Unaweza kujiuliza swali dogo kama wenye taaluma ya TEHAMA wanasambaza taarifa kama hizo Kwa umma na jamii nzima za kupotosha watu, je ni lini jamii itakuwa na hamasa na TEHAMA kama yule alie ambiwa asipo pata mtu wa kumweka sawa kuhusu jambo hili.
Sio mwalimu wa Tuition tu, kijana alieleza kwamba hata familia yake baada ya kuskia mawazo yake wamempiga vita sana na Hawaja onyesha ushirikiano wowote kwenye Hilo.
Ufahamu wa kompyuta Kwa matumizi ya kawaida
Mimi sifahamu chochote kuhusu taaluma ya mapigano yaani Martial Arts lakini Huwa naskia kwamba Kuna mikanda na ngazi kiasi kwamba ukiona mtu anamkanda flani katika pambano unajipanga na kumpimia pia unajiandaa Kwa kiasi gani ili umshinde na kama wewe unamkanda wa ngazi ndogo basi unajua kabisa kwamba Mimi kumpiga nitakuwa nimebahatisha sana.
Nimesema maneno hayo ili nijaribu kukuelimisha kwamba kwenye vitu vingi kuna ngazi za kujifunza mambo.
Ni ngumu sana kupima uelewa wako au kiwango chako bila kukutana na wengine kwenye jambo hilo ambao utapima kama umewazidi au wamekuzidi.
Ukipelekwa kwenye zizi la ng’ombe ukaambiwa chagua ng’ombe 10 Sina Imani kama utachagua ng’ombe dhaifu ninacho amini kwenye Hilo utachagua ng'ombe walio Nona.
Kama kuelewa uvumbuzi wa jambo na athari zake mbalimbali katika ulimwengu na jamii inayotuzunguka Kwa namna chanya ndio ukomavu kwamba sasa hili jambo elimu yake imeeleweka, Basi hata ukiamua kujifunza jambo kwenye TEHAMA unatakiwa utumie akili ya kawaida kama ulivyo tumia kuchagua ng’ombe 10 walio Nona.
Ufahamu wa kompyuta Kwa matumizi ya kawaida
Yaani itakubidi kutafuta sehemu ambayo TEHAMA imenona, TEHAMA imeenea na hapo ndio utapata matilio mengi ya kujifunza TEHAMA:
Kwa lugha rahisi wazungu ndio wenye maarifa mengi kuhusiana na TEHAMA kwenye vipengele vingi, Kwa hiyo ukitaka kujifunza taaluma hii ni vyema ukajifunza kutoka kwako, Kwa namna gani unaweza kujifunza kutoka kwako?? Jifunze Kwa internet, kama haujui kutumia internet tafuta maarifa ya internet kwanza.
Na ukihangaika kujifunza Kwa makala za kiswahili basi itakuwia vigumu na utazidi kupotosha jamii kwamba Kuna ugumu sana.
Tanzania yetu mwaka huu 2024 haijafikia kiwango kizuri Cha kuwa na makala za TEHAMA za kukufanya mtu flani kwenye TEHAMA na hata Kwa asilimia kubwa Bado jamii haielewi kuhusu uvumbuzi na athari za TEHAMA.
Na unayejifunza TEHAMA Sasa jikite sana kujifunza kutoka Kwa wazungu na ukifanikiwa kuelewa basi kuwa balozi mzuri nchini wa kusambaza mtazamo chanya kuhusu TEHAMA kwenye Tanzania hii ili mwisho wa siku tupate jamii yenye kuelewa uvumbuzi na athari za TEHAMA ili tuache kutegemea kujifunza kutoka Kwa wazungu, Kwani wao Wana vichwa na akili na sisi tuna vichwa na akili.
Ikiwepo jamii kubwa yenye kuelewa uvumbuzi na athari za TEHAMA basi ni rahisi sana na jambo la thamani kwenye Tanzania Kwa kutumia vipengele vingi kwenye TEHAMA.
Kama ilivyo rahisi kwenye kundi kubwa kupata maadui na marafiki hivyo hivyo kwenye jamii au kundi kubwa litakalo elewa TEHAMA kuzaliwa mambo mazuri na mabaya itakuwa rahisi na Kwa sababu Kuna viongizi wa nchi, mabaya yatazimwa na mema yatadumishwa kwenye TEHAMA ndani ya TANZANIANO.
Sio kama Tanzania yetu haina wataalamu hapana wapi ila Bado ni wachache kiasi kumpata sahihi wa kukuhamasisha kuhusu TEHAMA ni ngumu.
Waliopo wanatosha labda awe mwelekezi wako Hadi pale alipo fika yeye na ukisha fika hapo, ruksa unatafuta mwingine anaye zaidi hapo unajifunza yake yote ukimaliza unatafuta wa juu yake, ndio maana hapo awali nikazungumza kuhusu ngazi kwenye elimu nyingi zinazingatiwa.
Ufahamu wa kompyuta Kwa matumizi ya kawaida
Kwa yule anayeanza ni vizuri Kwa mwaka huu 2024 apate mwelekezi wa kibongo, Kwani ukiwa mbongo na unajaribu kujifunza TEHAMA Kwa mara ya kwanza utahangaika sana na makala za Kiswahili ambazo ndio nimesema hazijawa na kiwango Cha kukufukisha popote zaidi ya kukipa mwongozo tu, ni muhimu kutambua Hilo Kwani ukizikuta hizo za Kiswahili na ukaamini ni kwamba sasa ukimaliza itakuwa vizuri utakuwa unanidanganya peke yako kwa mwaka huu 2024.
Ukisha tambua kwamba unataka Kujifunza kuhusu TEHAMA, tafuta mwelekezi wa kibongo atakupa mwongozo mpaka uelewe wake unapoishia utaendelea na mwingine, mwingine na mwingine mwingine kuliko kujihangaikia mwenyewe.
Mimi nakuhakikishia utachukua muda mwingi na mrefu kujifunza jambo dogo kama hauna mwelekezi.
Kuna malengo mengi na vitu vingi sana ndani ya TEHAMA Kuna ujuzi mwingi sana hivyo ukitaka kujifunza TEHAMA ni vizuri ukatambua moja Kwa moja unaenda kujifunza jambo gani linalo weza kukipa mwanga wa mengine, japo wengi husema nataka kujifunza kompyuta akimaanisha anataka kujifunza TEHAMA.
Matumizi ya kawaida ya kompyuta nayo ni ujuzi mmoja wapo kwenye TEHAMA
Taaluma ya juu kwenye TEHAMA inajumuisha mambo mengi sana au taaluma nyingi sana, kabla ya kutaja chochote nitoe Lai hakikisha unachukua bahati ya kufanukiwa kujifunza haya kufuatilia katika vyanzo vingine ili kupata maelezo ya kina kutoka sehemu nyingi.
Utengenezaji wa akili bandia au programming ni moja ya ujuzi wa juu katika TEHAMA ambao unamtegemea mtu kujifunza lugha za kompyuta au lugha ya kompyuta ili kufanya hivyo.
Ujuzi wa mawasiliano, hii ni taaluma ya juu katika TEHAMA inayohusisha kuwezeaha miundo mbinu ya mawasiliano watu wenye taaluma hii wanaelewa undani kuhusu mitandao ya simu na jinsi minara unavyo fanya kazi.
Unaweza ukafahamu taaluma nyingi kwenye TEHAMA Kwa Kwa kutafuta katika vyanzo vingine pia
Mafanikio yanayofikiwa na watu wanaojifunza TEHAMA na kutambua fursa za pesa Huwa ni ya kuanza taratibu na Kisha kushamili sana yaani kipato kinakua kikikua Kila siku.
Ufahamu wa kompyuta Kwa matumizi ya kawaida
Kujifunza programming mafanikio yake ndio kama unavyoona Mitandao ya kijamii na Mifumo ya kompyuta kama Windows, Mac na Linux na Kwa bongo yetu kama unavyoona App ya Azam, Distv, Sportpesa,Bibilia, Quran, kwenye simu, Na unavyoona Tovuti ( website) na Mifumo kama Necta, Jamii forums, Tamisemi, MillardAyo.com
Unaweza kutumia ujuzi wa programming na taaluma ya juu ya umeme kutengeneza ROBOT au Mifumo mbalimbali ya automatic ya kujiendesha yenyewe kama unavyo ona taa za traffic barabarani na mashine za juu za ma Hospitalini, Bidhaa za Printer, kompyuta, kalukuleta na vitu kibao
Pia unaweza kuchukua muda kidogo kuperuzi mafanikio mbalimbali ya uvumbuzi na athari za TEHAMA kabla ya kujifunza TEHAMA Kwani hapa Mimi sija taja yote.
ZINGATIA:
ili uwe na uwezo wa kutengeneza program yenye uhalisia kutoka kwenye mawazo basi ni lazima uwe unafahamu programming language angalau moja.
Hiyo programming language moja ukiifahamu sio kama ndio itatosha kutengeneza programu kamilisha Bali lugha hiyo itajumuika na lugha zingine zitakazo hitajika kutengeneza programu hiyo:
Kwa nini ujifunze lugha moja wakati zitahitajika nyingi ??? Hii ni Kwa sababu kujifunza lugha nyingi Kwa wakati mmoja ni suala gumu lakini ukichagua kuelewa lugha zingine kadiri zinavyo hitajika katika matumizi yake.
Kwa mfano mimi nimejifunza na kufahamu JAVA programming language lakini katika development zangu natumia JAVA, PHP, MYSQL na zingine za ziada kama XML na JSON. Lugha nilivyo jifunza ni moja lakini nikaweza kutumia lugha hizo na ikawezekana .
Hivyo kujifunza lugha moja unaweza ukijaribu kujifunza development na ikawezekana Kwa maana Kila kitakacho hitajika utajifunza na kubobea mapema kutokana na uzoefu ulizo upata kwenye lugha mama yako.
Nahitimisha Kwa kusema sio wote wanaofahamu programming wanaweza kufanya development Kwa kiwango Cha taaluma zao, hii ni kutokana na kwamba hii ni taaluma ingine tofauti kidogo.
Ufahamu wa kompyuta Kwa matumizi ya kawaida
IMEANDALIWA NA JIKU TECH TIPS
Jiku Tech Tips ni Teknolojia ya kujifunza kutangulia inayojihusisha na masuala mbalimbali ya kidijitali.
Kupitia JIKU TECH TIPS unaweza upate ufanunuzi juu ya mambo mengi yanayo husiana na TEHAMA.
Jiku Tech Tips ni kama daraja flani au ngazi flani ambayo ukipita basi unakuwa unajiandaa kuwa mtu flani kwenye TEHAMA.
Huduma mbalimbali kutoka Jiku Tech Tips
- Android App Development ( Utengenezaji wa Application za simu za Android)
- Web Development ( Utengenezaji wa Tovuti na Programu zake )
- Mafunzo ya Java Programming Language FREE
- Mafunzo ya Software Development PREMIUM
- Uuzaji wa Vitabu vya Kujifunzia Teknolojia mbalimbali
Baadhi ya Bidhaa kutoka Jiku Tech Tips
- Kitabu Cha Utangulizi wa Android App Development Tsh 5,000/=
- Kitabu Cha Android Networking Tsh 5,000/=
- Kitabu Cha Kozi Kamili ya Android Development Tsh 10,000/=
- Kitabu Cha Mafunzo ya juu ya Kutengeneza Tovuti (website) Tsh 15,000/=
- Kitabu Cha Thamani ya Followers kwenye mtandao na jinsi unavyo weza kunufaika. Tsh 5,000/=
- Kitabu Cha Mafunzo ya matumizi ya namna ya kubobea internet Tsh 5,000/=
- Kitabu Cha ufahamu wa Compyuta Tsh 10,000/=
Mawasiliano:
Simu: +255 682 329 852
Email: jikutechtips@gmail.com
Blog: https://jikutechtips.blogspot.com
YouTube: Jiku Tech Tips
0 Comments