Android ni mfumo endeshi unaotumiwa sana kwenye vifaa vya kielectronic kama vile simu za mkononi na vifaa vingine vya kielectronic .
Utengenezaji wa application za simu za android ni mchakato wa kuunda na kuboresha programu za simu za android.
Application za simu za android zinaweza kuundwa na lugha mbalimbali za kompyuta kama vile Java, Kotlin n.k.
Kabla ya kuanza kujifunza Utengenezaji wa Application za simu za android ni muhimu sana kuwa na elimu ya msingi ya Application na uwezo wa kutumia lugha za kompyuta kama vile java,kotlin n.k ili iwe rahisi kubobea taaluma hii.
Kwa bahati mbaya changamoto kubwa inayo ikabili elimu hii ya utengenezaji wa application za simu katika nchi yetu ni kwamba elimu hii bado siyo rasmj katika taasisi zote zinazotambuliwa na serikali.
Elimu hii ipo ila haijapewa kipaumbele sana, kinyume kabisa na asili ya elimu hii inayo hitaji muda na nafasi kubwa ya kupambanua mambo na kufanya majaribio ili kuwa imara.
Kutokana na kwamba sio rasmi kumekuwa na ugumu mkubwa na ushirikiano mdogo wa jamii katika kueneza maarifa ya elimu hii kwani wimbi kubwa kwenye jamii yetu inaamini sana katika kauli, miongozo na mipango inayotolewa na serikali na kuamini vyanzo vya elimu nyingine ni utapeli.
Ni vigumu sana mtu mzima ambaye umri wake umeenda mbio kidogo kujishughulisha na elimu hii kwa sababu ya majukumu yanayo sababisha muda kuwa mchache ili kujihusisha na taaluma hii.
Pia, ni changamoto kwa kijana ambaye hujaanza kujitegemea kwani hawezi kumudu gharama ndogo za kujifunza kuhusu elimu hii hasa bando la INTERNET, kwa sababu ya kutegemea uchumi kutoka kwa mzazi , mlezi au mfadhili wake.
Hata hivyo baadhi ya vijana ambao wamepata bahati ya kuwa na uwezo wa kujitegemea inawawia vigumu sana kutoa muda wakutosha kuhangaika na taaluma hii yenye utajili, kwa sababu wakiacha shughuli zinazo wapa kipato cha kila siku maisha yataendaje bila kipato??? Swali ambalo imekuwa ni gumzo kwa wengi kuchukua maamuzi ya kujifunza elimu hii ambayo ni miongoni mwa elimu nyingi ndani ya ulimwengu wa TEHAMA.
Nitoe lai kwa mfuatiliaji ambaye ni mpya ambaye amebahatika kupata makala hii ya kipekee, kabla ya kujifunza au kufahamu upana na ukubwa wa fursa za TEHAMA zilizomo ndani ya elimu hii ya utengenezaji wa application za simu, kuwa apate muda mwingine wa kupitia elimu ya fursa mbalimbali za kidijitali katika ulimwengu wa kiteknolojia kwenye vyanzo mbalimbali vya elimu kwenye ulimwengu wa TEHAMA kama vile YouTube, Facebook , Google Search, Instagram,X(Twitter) na blog au tovuti zenye elimu hiyo
Ewe mzazi ulie pata bahati ya kuelewa habari hii elimu hii miongoni mwa elimu nyingi zilizopo kwenye TEHAMA zinaweza mpa uwezo kijana wako wa khjitegemea mapema sana na kuona matunda bila ya kuajiliwa na serikali kama ilivyo zoeleka tangu zamani yaani kuishi kutegemea Ajira kutoka serikalini .
Unaweza ukatamani kufahamu elimu ya utengenezaji wa Application za simu lakini ukakosa muongozo sahihi.
Muongozo sahihi na muongozo mzuri bahati mbaya haulatikani kwenye Elimu rasmi yaani elimu serikalini, bali muongozo unaweza kuwa mzuri kwa kuboresha au kuanza kujifunza elimu hii upo kwenye vyanzo ambavyo jamii yetu inatambua kuwa sio rasmi kiasi kwamba hata ukimweleza mzazi , mlezi au mfadhili anae weza kilipia gharama ndogo ni ngumu kuelewa habari kama hii kutokana na ugeni wa elimu hii katika fikra za watu wengi kwenye jamii yetu ya Tanzania.
Ni dhahili na inawezekana nguvu ya kujifunza jambo au kufanya jambo au kupigana na jambo kwa mtu , inatoka kwa mtu mwenyewe.
Jiunge na wabunifu wa teknolojia ujifunze mambo yanayo weza kujenga nguvu ndani yako ya uwezo wa kubobea elimu ya utengenezaji wa Application za simu za android kwa ajili ya manufaa yako.
Katika kutambua mambo mengi JIKU TECH TIPS imeandaa elimu ya utangulizi wa utengenezaji wa application za simu za android katika kitabu cha UTANGULIZI WA KUTENGENEZA ANDROID APPLICATION hata kama wewe ni mpya.
Katika kitabu utapata elimu na siri kubwa za kuunda application za simu za android za kuvutia watumiaji kuanzia mwanzo hadi ufundi wa hali ya juu.
Pamoja na muongozo unaopatikana kwenye elimu ndani ya kitabu hicho vilevile utajifunza jinsi ya kubuni Application zenye nguvu na za kuvutia watumiaji.
Hivyo hakikisha unachukua nafasi hii ya kipekee kuchimba dhahabu ya fursa katika ulimwengu wa utengenezaji wa Application za Android.
Usikose fursa hii ya pekee ya kujiongezea maarifa na ustadi wa kipekee katika ulimwengu wa teknolojia ya kisasa.
Gharama ya kitabu ni Tsh 5,000/= .
Kitabu unakipata kwa njia ya WhatsApp baada ya kufanya malipo kwenye namba ya simu 0682329852. Yenye jina ALEX NCHINGA.
Kama wewe ni mpenzi wa makala za namna hii nikuambie asante kwa muda wako t
ukutane muda mwingine katika makala zingine.
0 Comments