Jiku Tech Community
Jinsi ya kujipatia kipato kwa njia ya mtandao
Zipo namna nyingi za kujipatia kipato kwa njia ya mtandao ila sasa kwa kua sisi ni waswahili njia zingine siwezi kuziongelea sana zaidi nitaongelea kupata pesa kwa njia ya matangazo
Unalipwa kwa kuonesha matangazo ya kampuni flani kwenye aidha website yako, blog yako , youtube channel yako au android app yako
Kama haufahamu unaweza ukawa unajiuliza
Website nini?
Blog ni nini?
Youtube channel ni nini?
Android app nini ?
Website na Blog havina utofauti mkubwa sana katika matumizi ya kuonesha matangazo kwa ajili ya kulipwa .
Youtube channel ni kama television ambayo mmiliki anajukumu la kutafuta watazamaji wa kudumu na mala baada ya kuwapata wadau hao (watazamaji) ndipo mmiliki huanza kulipwa na makampuni atakayo omba matangazo kwa ajili ya kuyaonesha kwa wadau wake kupitia television yake (youtube channel)
Android app
Hizi ni app kama zile zinazo onekana playstore
Wamiliki
Ma Developer
Wa Wekezaji
Ma developer hawa ni watu wanao tengeneza applicstion wenyewe kwa kutumia software maalum zilizotengenezwa na wazungu kwa ajili ya kutengeneza program mbalimbali software hizo mfano ni android studio, visual studio code, intel j na mfano wa program zinazotengenezwa na software hizi ni
App ya branch , tala , ma Game ya kwenye simu
Wa wekezaji hawa ni wale ambao wao wananunu app Fulani mara tu baada ya kuona fursa katika wazo Fulani ambalo linaweza kuwa hadharani kama mobile app
Kwa sasa nitajikita sana kuelezea ni kwa namna gani unaweza kujipatia pesa mtandaoni kwa kupitia kumiliki moja ya vitu nlivyo taja hapo juu hususani Mobile Application
Mchakato Wa Kupata Pesa Kupitia Mobile App
o Hatua Ya Kwanza Ni Wazo
o Hatua Ya Pili Ni Kumiliki Mobile App Haijalishi Umetengeneza Wewe Au Umetengenezewa.
o Hatua Ya Tatu Ni Ku Publish Mobile App Katika Soko La Playstore Ambapo Lazima Uwe Na Akaunti Ya Google Play Console Ambayo Inakuwa Na Uwezo Wa Kupublish Mobile App Zaidi Ya Moja. Akaunti Hii Gharama Ya Kuifungua Ni Takribani Dollar Za Kimarekani 25$ Ambazo Unalipa Kupitia Laini Ya Simu Yako Kwa Njia Ya Mastercard.
o Hatua Ya Nne Ni Kufanya Promotion Mara Ya Baada Yak U Publish Mobile App Yako Kwenye Soko La Playstore ,Kama Unaona Ugumu Wa Kufanya Hivyo Kuna Makampuni Na Watu Binafsi Wanfanya Kazi Ya Promotion Ya Vitu Mbalimbali Mtandaoni Unawalipa Kiasi Kidogo Cha Pesa Wanafanya Kwa Niaba Yako.
o Hatua Ya Tano Na Ya Mwisho Ni Kujisajili Na Kampuni Maarufu Ya Admob , Kampuni Ambayo Watakulipa Kwa Kuweka Matangazo Yao Kwenye Application Yako .
Baada ya kusoma na kuelewa napenda kujulisha kwamba kazi au fursa za mtandaoni ni kazi ambazo jasho linakutoka mara tu unapoanza lakini zikisha anza kuingia pesa ni hata kama umelala asubuhi ukicheki dashboard yako unaona kama zimeongezeka , hivyo ni aina flani ya uwekezaji ambao mlolongo wake ni maneno macheche tu kama haya lakini matokeo yake ni makubwa
Chakufanya kama umependezwa ukitaka kupata pesa kwa njia hii jifunze kutengeneza mobile app kwa kutumia software kama nlivyo kutajia hapo juu, kwa maana kujifunza ni kitu ambacho kitakuchukua mda mrefu kidogo basi njia rahisi ni kutafuta wazo zuri litakalo fanya vizuri sokoni na kumtafuta mtengenezaji kwa ajili yakukutengenezea mobile app kutoka kwenye wazo lako.
Mwisho nipende kukufahamisha kwamba jiku tech community ni jumuiya yenye wataalamu wengi wenye uzoefu na ueredi mkubwa katika masuala ya
· Mobile app development,
· Web development and
· Blog making
Jinsi ya kupata pesa mtandaoni
Jinsi ya kutengeneza email
Jinsi ya kuingia kwenye email yako ya zamani
Blogging na pesa mtandaoni soma kwa makini
Mafunzo ya computer kwa kiswahili
Aina za computer
Nini maana ya database
Prepared by Jiku Tech Community
Simu : 0682329852
0 Comments