Umejifunza kuhusu method kwamba method zinakuwa declared kwenye class na kuwa zinatumika kufanya jambo flani.
mfano:
tengeneza method iite myMethod()kwenye Main class
public class Main {
static void myMethod(){
System.out.println("Hello world");
}
}
myMethod ina print neno " Hello world" pindi tu inapotajwa na hiyo ndio kazi ambayo imepewa
ili kuitaja method andika jina la method , ikifuatia na mabano ya aina hii () na nukta pacha za nusu (;)
mfano:
ndani ya main taja myMethod();
public class Main{
static void myMethod (){
System.out.println("Habari");
}
public static void main(String[] args) {
myMethod();
}
}
// output Habari
static vs public
itakuwa mara nyingi sana kwenye program za java utaona neno static na public
kwenye attributes na methods
kwenye mfano uliopita tulitengeneza static method na ambayo ina maaana kuwa tunaweza kuitaja hata bila kutumia object ya class yake
tofauti na public ambayo kuitaja mpaka utumie object ya class yake.out
mfano:
public class Main {
// static method
static void myStaticMethod(){
System.out.println(" static method inatajwa bila object");
}
//public method
public void myPublicMethod(){
System.out.println("public method kutajwa lazima object");
}
// main method
public static void main(String[] args) {
myStaticMethod(); // tumeitaja static method
Main myObj = new Main();
myObj.myPublicMethod (); // tumeitaja public method kwenye object
}
}
Access methods with an object
mfano
tengeneza object ya Gari ipe jina gariYangu taja fullThrottle() na speed( methods za object ya gariYangu kisha run programu yako.
//tengeneza Main class
public class Main {
// tengeneza fullThrottle() method
public void fullThrottle(){
System.out.println(" gari inakimbia iwezavyo");
}
// tengeneza method ya speed kisha pitisha parameter
public void speed(int spidiyajuu){
System.out.println(" speed ya juu ni : " + spidiyajuu);
}
// ndani ya main taja method zote kwenye object ya gariYangu
public static void main ( String [] args){
Main gariYangu = new Main(); // tumetengeneza object ya gari yangu
gariYangu.fullThrottle(); // tumetaja fullThrottle() method
gariYangu.speed(200); // tumetaja speed() na kupitisha argument - 200
}
}
// output: gari inakimbia iwezavyo
// output: speed ya juu ni : 200
Maelezo ya mfano
Tumetumia keyword ya class kutengeneza class yetu ya Main.
tumetengeneza fullThrottle() na speed() method ndani ya Main class
Tumefanya fullThrottle() na speed() method hizi zi print maneno flani pindi zinapo inapotajwa
Tumetengenza method ya speed () ikubali kupitisha parameters ambayo ni tarakimu inayo itwa spidiyajuu
Ili tuweze kutumia Main class na method zake inabidi tutengeneze object ya Main class
Nenda sasa kwenye main () method ambayo mpaka sasa ni method ipo ndani ya java language ambayo kazi yake ni ku run programu yako ( yaan code zozote ndani ya main() zinakuwa executed)
Kwa kutumia keyword ya new tumeweza kutengeneza object yenye jina gariYangu
Kisha baada ya hapo tumetaja fullThrottle() na speed() method hizi kwenye object ya gariYangu na tuka run programu yetu kwa kuandika jina la object (gariYangu), ikifuatia na dot(.),ikifuatia na jina la method ( fullThrottle(); na speed(200);) na kumbuka tumeongeza parameter ya 200 ndani ya method ya speed().out
ZINGATIA:
alama ya dot (.) hutumika ku Access attributes na methods za object
Java Constructors
kama wewe ndio mara ya kwanza kujifunza kuhusu java programming language kuanzia hapa ongeza hali ya kuzingatia
kwani bila kufanya hivyo unaweza ukapata changamoto kidogo pindi tutakapo anza kujifunza development
Constructors kwenye java, hizi ni kama method maalumu ambazo hasa hutumika kufanya initialization ya object yako kwenye masomo yaliyo pita tulijifunza kuhusu ku declare na ku initialize
mfano
int x;
Hapa maana yake nime declare kwamba katika programu yangu nitakuwa na variable ambayo itaitwa x, japo thamani yake bado haujaweka, baada ya kuandika int x;
Mstari unaofuata niandike x =5; hapo nitakuwa nime initialize yaani nimethamanisha x = 5; value ya x tayari inajulikana katika programu,
Sasa kwenye Constructor tunaposema constructor ni method za ku initialize object maana yake utaielewa kuanzia hapa.
Pia nimesha sema nikama method ila yenyewe ni maalumu yenyewe kuitaja kwake ni tofauti na method za kawaida na ninaposema kutaja na maanisha ku Call
pindi tu unapotengeneza object ya class ambayo ndani yake kuna constructor basi constructor inakuwa called
Ili ugundue hilo utaona kwenye IDE yako baada tu ya kutengeneza object basi inakuletea error kwamba lazima uweke attribute/ argument kama inavyotakiwa kwenye class inayotokea
mfano:
tengeneza constructor
// tengeneza class
public class Main {
int x ; // tume declare variable
// tengeneza constructor ya Main class
public Main() {
x = 5; // tume initialize value kwa attribute x ya class Main
}
public static void main(String[] args) {
Main myObj = new Main(); // tumetengeneza object ya class Main ( kwa kufanya hivi tume i call constructor)
System.out.println(myObj.x); // tuna print value ya x
}
}
// output 5;
ZINGATIA:
- jina la constructor lazima lifanane na jina la class ilimo na haina return type ( kama void)
- vilevile kumbuka kuwa constructor inakuwa called pale unapotengeneza object ya class ilimo
- kitu kingine cha muhimu kujua ni kwamba classes kwenye java huwa zina constructor hata kama haujatengeneza
Constructor parameters
Pia kama nilivyo eleza hapo awali kwamba constructor zinapitisha parameter kwa namna ile ile kama methods
parameters ambazo zinatumika ku initialize attribute za classes
mfano ufuatao utaongeza int y parameter kwenye Constructor , ndani ya constructor tume set x iwe y ( x= y )
Pindi tunapo call constructor lazima tupitishe parameter kwenye Constructor ambapo kwenye mfano tumepitisha (5) ambayo ita set value ya x kuwa 5
mfano
public class Main {
int x;
public Main (){
x=y;
}
public static void main(String[] args) {
Main myObj = new Main(5);// kama hiyo tano isipo wekwa basi ita compaili error
System.out.println(myObj.x);
}
}
// output: 5
Vilevile unaweza kuwa na parameter nyingi kwa kadiri ya matumizi yako
mfano
public class Main{
int modelYear;
String modelName;
public Main(int year, String name){
modelYear = year;
modelName = name;
}
public static void main(String[] args) {
Main myCar = new Main(2024,"toyota");
System.out.println( myCar.modelYear + " " + myCar.modelName);
}
}
// output 2024 Toyota
Mwisho wa somo hili la 15 Nipende kila mmoja kwa faida yake aingie Google ajifunze kuhusu " Java Modifiers"
0 Comments