Java encapsulation
Maana ya encapsulation ni kuhakikisha data nyeti zinafichwa kwa mtumiaji na ili kukamilisha hili unatakiwa ku
- ku declare variables / attributes kama private ( private ni modifier kama ulivyo jifunza kutoka Google)
- weka public get na set method za ku access na ku update value za private variables/attribute.
Get na Set
umejifunza kwenye access modifier kwamba private variables zinaweza kuwa accessed ndani ya class zilimo tu na
class ya nje yoyote haiwezi kuzifikia, Lakini inawezekana kuzifikia ikiwa utatengeneza public get na set methods
get method yenyewe ina return value ya variable
set method yenyewe ina set value
syntax
- kama ni get basi itaanza na get,bila kuacha nafasi ikifuatia na jina la variable,
jina la variable herufi ya kwanza iwe kubwa
- kama ni set basi itaanza na get,bila kuacha nafasi ikifuatia na jina la variable,
jina la variable herufi ya kwanza iwe kubwa
mfano:
Maelezo ya mfano
get method ina return value ya variablename
set method inachukua parameter (newName) na ku i thaminisha kwa name variable , na hapo
utaona kuna this keyword ambayo inatumika ku refer Object ya muda huo
na vile vile variable ya name itakuwa declared kama private na hivyo hatuwezi kuipata nje ya
class ilimo.
mfano huu uta run Error
kama tangekuwa tume declare variable kama public basi majibu yangekuwa
output: John
ili kupata majibu hayo hata kama tumetumia private tunatakiwa kutumia getName() na setName()
ku access na ku update variable
mfano:
Kwa nini encapsulation
- Ubora kwenye kudhibiti attribute na method za class
- programmer anaweza kufanya mabadiliko ya code kwenye sehemu moja bilia kuathiri sehemu
ingine.
- ina ongeza usalama wa taarifa
Java Packages
Package kwenye java hutumika kuweka makundi ya class zinazo husiana kama unatumi smartphone au computer fikilia kama folder ambalo linakuwa na files mbalimbali mfano movies zako si linakuwa kwenye folder moja.
package zinatumika ili kuepusha mchangamano wa majina na kuandika code ambazo zinaweza kudhibiti kiurahisi
package kwenye java zimegawanyika katika makundi mawili
- Built-in Packages ( package kutoka kwenye API za java language)
hizi ni package ambazo zimesha tengenezwa wakati wa uundaji wa java programming language
hivyo ni kuzitumia tu.
- User defined Packages (unajitengenezea mwenyewe)
hizi ni package ambazo mtu anatengeneza mwenyewe
Built-in Packages
hapa ni muhimu kuhusu library ,, library ni mkusanyiko wa packages
ili kutumia class au package kutoka kwenye library unatakiwa kutumia keyword ya import
syntax
Import a Class
kama ukipata class unayotaka kuzitumia mfano Scanner class ambayo ni built-in class inayotumika
ku chukua taarifa kwa mtumiaji andika code zifuatazo:
import java.util.Scanner;
kwenye mfano hapo juu java.util ni package wakati Scanner ni class ipo ndani ya
java.util package
Kama kawaida ili kutumia Scanner class tengeneza object ya class hiyo na hapo unaweza
kutumia method yoyote inayo patikana kwenye Scanner class. na ndani ya class hii
zinakuwepo method nyingi unaweza ukatumia google kutafuta method zote ambazo zipo kwenye class flani ya java mfano "list of all method in java Scanner class " kwa kuandika hivi kwenye google
utapata orodha ya method zote zilimo kwenye Scanner.
Kwenye mfano tutatumia nextLine() method ambayo husoma mstari wote
mfano:
kwa kutumia Scanner class kupata taarifa za mtumiaji
import package
unaweza kuchagua kutoka kwenye package nyingi sana, kwenye mfano
uliopita tulitumia Scanner class kutoka kwenye package ya java.util package
hii inabeba utility nyingine nyingi kama tarehe na utility class nyingine
ili ku import package kama tulivyo jifunza hapo awali tumia alama ya nyota (*)
mfano
Java Inheritance (sub class na super class)
inheritance maana yake ni urithi
Kwenye java inawezekana ku inherit attribute na methods kutoka kwenye class moja kwenda nyingine
Nadhalia ya inheritance tunaweza kuigawanya katika makundi mawili
- subclass (child) class ambayo ina inherit kutoka kwa ingine
- superclass (parent) class ambayo ina kuwa inherited.util
Ili ku inherit class flani tumia keyword ya extends.
Kwenye mfano hapo chini class ya Car ambayo ni subclas ina inherit attribute na methods kutoka kwenye class ya Vehicle ambayo ni Superclass
mfano
Hapa ndio mwisho wa somo la 16 na mwisho wa nadhalia ya java programming language usije usahau ukasema umesha bobea java programming language kwa kupitia masomo haya 16 ni kweli utakuwa na kiwango flani kwamba unafahamu java ila kinacho hitajika sana ni mazoezi na ufuatiliaji wa mambo kwa undani wake
Tulimejifunza haya ili kuepusha mtu kuchanganyikiwa na baadhi ya mambo wakati wa
kujifunza Software development kwani Mission ya Jiku Tech Tips ni kufundisha mtu yoyote
anaye jua kusoma na kuandika ikiwa tu ana nia na malengo flani kwenye Tehama na hasa
utengenezaji wa Software ambazo zinaweza kusaidia jamii na yeye mwenyewe binafsi
kwenye shughuli mbalimbali kwa ajili ya kujipatia kipato.
Jiku Tech Tips haifundishi mtu kama shuleni imejikita kumpa mtu uwezo wa kutengeza Software sio kumfundisha, kama unavyo fahamu kiwango cha akili huwa kinatofautiana ukipewa uwezo kidogo ukatumia vizuri kwa kiwango chako chote cha akili ulizo pewa na mwenyezi mungu inawezekana ukampita
hata yule aliye kupa. Jiku Tech Tips ita kuhusia kwamba kuna jambo flani katika Software development linapatikana na kufanywa hivi na manufaa yake ni haya.
Ili kuendelea vizuri tazama video hii HAPA, Baada ya kutazama video pitia maelezo ya kujiunga na mafunzo rasmi ya Software Development HAPA
0 Comments