Maelezo ya Kujiunga na Mafunzo ya Android Development
Karibu katika safari ya kujifunza kutengeneza android app yaani App za simu za Android, Kujifunza Taaluma hii kuna umuhimu wa mtu kuwa na uelewa wa nini anaenda kufanya na kwa nini.
Elimu hii ni moja kati ya elimu ndani ya software development, kwa hiyo kwa kutekeleza mafunzo haya ya utengenezaji wa android application utakuwa na uelewa wa juu wa maana ya Software development.
Mahitaji
Lazima mtu anaejifunza taaluma hii awe na ujuzi wa lugha ya compyuta (programming language ) angalau moja. Zipo lugha nyingi zinazowezesha kufanikisha taaluma ya utengenezaji wa android application na unaweza kujifunza moja wapo ili kuendelea na taaluma hii, kama hauna ujuzi na lugha yoyote unaweza kuchukua muda kidogo kujifunza kwenye vyanzo mbalimbali mtandaoni japo inakuwa ngumu kidogo kwa sababu ya kiingereza cha kiteknolojia hivyo kama utakutana na ugumu huo unaweza kurejea mafunzo kutoka Jiku Tech Tips ya Java Programming Language ambayo yamegusa vipengele vyote vinavyoweza kuhusika katika kutengeneza android app kwa kutumia lugha ya java, na ikiwa tayari umesha hudhulia mafunzo hayo basi uko tayari kuendelea.
Lazima uwe na compyuta.
Lazima uwe na uwezo wa kununua bando angalau 2Gb - 5Gb.
Lazima uwe na muda.
Programu au kifaa au Software inayo tumika kutengeza software/programu katika taaluma hii tunauo jifunza hapa na zingine, jina maarufu huitwa SDK neno ambalo ni kifupisho cha maneno Software Development Kit.
Kwahiyo ili kufanisha mchakato wa kutengeneza Programu au Software za simu za Android ni lazima tuwe na SDK maalumu, ambapo katika safari yetu tutatumia Android Studio kuzalisha android app.
SDK ni kama box linalobeba zana mbalimbali zinakamilisha uzalishaji wa Android App, hivyo ni lazima kabla hatuja jifunza mambo ya juu tupate uzoefu wa kutumia Android SDK kwa kufanikiwa kufanya mazoezi mengi ya aina mbili.
Aina ya kwanza ya mazoezi mengi ni kufanikisha ku run App ya kwanza kwenye simu ambayo ukiifungua kwenye simu yako ita kuonesha maneno “ Hello World”, dhumuni la zoezi hili nikujirisha kama SDK yako imejikamilisha kila kitu kwa ajili ya kuzalisha app, na kwanini nasema imejikamilisha, SDK huwa na tabia ya ku download vifaa pendwa kwa kadiri inavyo hitaji yenyewe, cha msingi ni uwe na bando la internet ili ifanikiwe kujikamilisha.
Aina ya pili ni kufanikisha kubadilisha tovuti (website ) kuwa android app kwa kutumia source code za watu wengine mtandaoni yaani kuzi copy na kupaste na kuzipangilia ili zi run bila tatizo. Dhumuni la zoezi hili ni kukujengea uelewa kwamba hutakiwi kuhangaika muda mwingi kuunda kitu ambacho kimesha undwa na badala yake nikuwa lengo lako litimie na uwe na uwezo wa kuthibiti kila kitu, yaani maana yangu ni kwamba sio eti kwa sababu umejifunza java basi ndio lazima muda wote utengeneze code zako , haitakiwi ivo ni kupoteza muda au ni sawa na eti unajua kupika chapati basi muda wote ili ule chapati upike wewe muda mwingine unaweza usiwe na nafasi ukala za kununua au ukaingia kwa jilani kula bure na ukatumia ujuzi wako wakujua kuzipika kujua ni bora au sio bora.
Masomo au mazoezi hayo ya aina mbili yatatupa uzoefu wa kutumia SDK
Baada ya kupata uzoefu ni muda sasa wa kutengeneza programu kwa jinsi mtu unavyo taka wewe kama utaamua kuunda calculator kama utaamua kuunda duka la mtandaoni ni wewe, kama utaamua kuunda app ya kutunza taarifa flani ni wewe.
Ili ufanikiwe kuunda programu lazima upate elimu ya kuunda programu kwa vitendo yaani unaanzaje anzaje mpaka inakuwa app kama mtu ulivyo waza ??
Mimi huwa napenda kuandika mawazo yangu kwenye karatasi au daftari kabla zijaanza kuunganisha ili kuunda programu.
Tutajifunza taaluma ambayo itafungua uelewa wa namna ya kufanya development kwa nadhalia maarufu sana kwa kiingereza inaitwa CRUD Operation , CRUD ni kifupisho cha maneno:-
C - Create
R - Read
U - Update
D - Delete
Nadhalia hii itafanya kubobea na kuelewa mambo mengi sana kwenye somo la software development somo hili kwa ujumla wake ingawa tutakuwa tunajifunza kipenge chake kimoja cha Mobile App Development.
Katika kutekeleza nadhalia hii tutatumia programming language zaidi ya moja ili kufanikisha mchakato ambazo ni PHP na MYSQL.
Na baada ya kukamilisha nadhalia hiyo utakuwa na uwezo wa kutatua changamoto nyingi sana kwa kutumia Programming za kwako na za wengine kwa manufaa yako.
MAFUNZO
Baada ya kuelezana mambo haya ya msingi karibu sasa katika mafunzo rasmi.
Mafunzo yameganyika katika level tatu Msingi, Secondary na Advanced
Masomo katika level ya Msingi
Namna ya kudownload , ku- install android studio na jinsi ya kutengeneza project ya kwanza.
Namna ya kuunganisha smartphone na android studio
Namna ya kubadilisha website kuwa android app
Masomo katika level ya Secondary
Ufahamu wa Object Oriented Programming (OOP) kwa kutumia java programming language
Masomo katika level ya Advanced
Android networking
Database structure
CRUD Operation
Gharama za Mafunzo
Vitabu
Namba ya Malipo ni 0682 329 852 yenye Jina ALEX ANOD NCHINGA namba ya mtandao wa Airtel.
Mafunzo ni kwenye mtandao kwa kutumia programu hizi ambazo zinatakiwa kuwepo kwenye compyuta yako.
Any Desk
Bandcam
Android Studio
NetBeans au Eclipse IDEs
ANY DESK
Hii ni screensharing Program ambayo inatumika kufanya muunganiko wa vifaa kwanzi viwili kwa ajili ya kuelekezeana jambo flani live.
BANDCAM
Hii ni Screen Recording Program ambayo inatumiwa na mwanafunzi kurecord video ya kipindi kinacho endelea kwa ajili ya kumbukumbu.
ANDROID STUDIO
Hii ni Software Program ambayo inatumika kutengeneza Program za Simu.
NETBEANS / ECLIPSE IDEs
Hizi ni Program ambazo zinatumika kujifunzia Java Programming Language kwa vitendo kabla ya kufanya project ya uhalisia.
Piga namba Hii kama nahitaji msaada
0682329852
0 Comments