Nimeshudia watanzania wengi wanamaliza taaluma zao vyuoni na kwa bahati ya wachache kubahatika kupata ajira mapema tu mara baada ya kumaliza taaluma zao.
Wanamaliza wengi kila mwaka lakini wana ajiliwa wachache sehemu tofauti tofauti. Vip kama sio wewe uliye ajiljwa??
Zaidi nililenga ma IT
Je, Umesoma , Unasoma au upo interested na taaluma ya IT ???
Hii ni kwa ajili yako.
Wengi wanao kuwa chuoni hawana uwezo wa kujitegemea, mara nyingi hupata kibuli cha kuongea kwa uhakika kwamba nitafanya ivi na vile wakisahau in charge wa gharama zao za maisha ya muda huo.
Hasa in charge ni wazazi au walezi au taasisi au mkopo.
Na mara baada ya kumaliza masomo
In charge hao hawana tena sababu ya kutoa fedha zao , zaidi ya kukaa na kuskilizia mambo kibao kutoka kwako kwamba alijifunza nini huyu mtu.
Kama IT unawezaje kujiajili katika tehama. ??
Baada ya kumiliki ujuzi wa TEHAMA
Unatakiwa kujikumbusha maana na ujio wa TEHAMA kwenye ulimwengu.
Itakusaidia kujenga ushirikiano wa mambo kwenye jamii.
Lengo mojawapo la TEHAMA kwenye ulimwengu ni kurahisisha mambo.
Pesa ni kipaumbele sana katika kuishi je unafanyaje sasa TEHAMA ikupe fedha ???
Kaa chini na utafakali aina zote za shughuli wanazo fanya watu na kujipatia kipato cha kila siku.
Tafakari namna na ufanywaji wake izo shughuli.
Bila shaka utagundua analogue inahusika sana zaidi ya dijitali.
Rudi kwenye lengo la TEHAMA (kurahisisha mambo) fanya biashara ambayo unaiweza kwa kutumia TEHAMA yaani irahisishe kwa kutumia tehama .
Namaanisha nini hapa ???? Sio kwa sababu umesoma TEHAMA ndio ufanye biashara ya computer, utangaze kwamba unatengeneza mifumo mara unafanya design ya kitu gani sijui mambo kibao!! HAPANA !!!
MFANO:
Uhusiano wa Biashara ya nguo na TEHAMA.
Kwanza ni dhahili kwamba kunawatu wanaendesha maisha yao kupitia biashara hii. Tuchukulie kipengele cha software development kwenye TEHAMA. Kama kweli umesoma taaluma hiyo kwa nini usitengeneze mfumo unao weza kukusaidia kufanya biashara hiyo , kama vile kuzipa bidhaa identification number (ID)kisha kuziweka kwenye mfumo ambao mtu anaoda kwa ID na aki order sharti alipie kidogo akisha lipia Bidhaa aliyo lipia inatoka hewani kwa ajili yake.
Kwa Nini nimetolea mfano biashara ya nguo maana yangu kubwa kuliko u quit taaluma yako na kuachana kabisa bora utafute namna ya kuhusisha na chochote utakacho amua kukifanya mtaani kwa sababu ukifanya hivyo mafanikio yanakuwa makubwa kuzidi yule ambaye anafanya biashara hiyo hiyo kiholela.
Hii ndio wale ma in charge huwa wanakaa na kuskilizia huyu mtu atafanyaje. Huwa wanafarijika sana ukiwa mbunifu .
Wengi ambao huwa wanaliona pengo la TEHAMA kwenye shughuli zao mara nyingi huwa wanatamani kujifunza kipengele wanacho kilenga kwenye TEHAMA kutokana na shughuli zao.
Wale ambao wanasoma taaluma hizi huwa wanajiona wanaweza kila kitu ila kufanya wanshindwa.
0 Comments