Nini maana ya AI
Ni akili ya mashine au program kinyume na akili ya binadamu au wanyama
Kukua kwa sayansi na technology kimewezesha uvumbuzi wa vitu vingi sana
Fikiria mtu anavyo zaliwa maana yake ana empty mind yaani akili yake inanakuwa haina hata kumbukumbu moja wala uzoefu wowote ule wa kufanya jambo lolote lile lakini kadri amtu huyu anavyo kuwa anakuwa ubongo wake unakuwa unajifunza mambo mbalimbali ambayo ni msingi wa utambuzi wa mambo mengine
AI kwa kiingereza ni Artificial intelligence
Mtu yeyote anaweza tengeneza machine ambayo ina fanya utambuzi wa mambo flani kwa kadri atakavyo taka yeye
Mtu huyu atakuwa na kazi ya kutengeneza machine baada ya hapo atakuwa na kazi ya kuifundisha michakato ya kukamilisha majukumu anayo itaka ifanye
Machine ikisha fundishwa basi inabaki inasubuli amri tu kwamba fanya hivi
Nna imani umewahi kuskia habari ya robot
Robot wapo wa aina kama mbili kwa jinsi ninavyo elezea maana yangu hapa
Robots wa aina ya kwanza ni wale wanao shikika na wale wasio shikika
Mfano wa robot anaye shikika ni kama printer na wale unao waona kwenye movie kwamba huyo roboti kazi yake ni kuchukulia mgeni maji ya kunywa pindi anapo amrishwa kufanya hiyo kazi
Robot wa aina ya pili ni robot ambaye haishikiki robot hawa ni wengi sana kwenye ulimwengu huu wa leo kiasi kwa asilimia mia moja unao hapo ulipo
Mfano wa robot hawa wasio shikika ni kama App ya kumpigia mtu simu yeye anatekeleza amri na mambo yote yanayohusiana na kupiga na kupokea simu
Tulikuwa tunajifunza kuhusian na AI
Ambayo kiufupi ni akili bandia inayo tengenezwa na kuwekwa kwenye machine kwa ajili ya jukumu au majukumu flani kulingana na matakwa ya mtengenezaji wa program hiyo
Utendaji kazi wa Ai
Huwa ni kupokea amri kutoka kwa m tumiaji na kuichakata kwa namna ya maelekezo ambayo ndio akili aliyo wekewa
Nani anatengeneza akili bandia
Mtengenezaji wa akili bandia ni yule mtu alie jifunza software engineering kwa undani sana
PIA UNAWEZA JIFUNZA ZAIDI HAPA
0 Comments