MUONGOZO WA PROGRAMMING NA UTEKELEZAJI WAKE KATIKA MAZINGIRA HARISI.
SOFTWARE ENGINEERING
Ni taaluma ambayo inatumia kanuni za uandisi (engineering principal) ku design, kutengeneza,kuboresha , kujaribisha na pambanua mifumo ya software ambayo ina ruhusu compyuta kufanya utendaji mbalimbali
Watu hawa hufanya kazi ya kutengeneza software ambazo ni suluhisho kwa matatizo mbalimbali kwa kutumia tasnia nyingi kwenye ulimwengu wa Tehama kama vile
- Web development
- Mobile app development
Software engineer wana ujuzi wa programming na ujuzi wa hatua za kutatua tatizo flani kwa umahili wa Haliya juu sana.
Ili uwe software engineer lazima ujifunze programming languages mbalimbali kama vile Java, python, c++ n.k na vile vile nadhalia mbalimbali kama vile
- Data structure
- Algorithms
- Object oriented programming
Jiku Tech Tips itaanza kwa kuangazia zaidi Object Oriented Programming (OOP) .
Object Oriented Programming ni mbinu ya kuandika na kupangilia programs na inaweza tekelezwa na programming language ya aina yoyote iwe Java, Python, C++ n.k
Huu ni mfano ambao utakufahamisha zaidi kuhusiana na OOP
Mfano
Unaweza tembelea kibanda cha computer ambacho huwa wanafanya kazi ya kutengeneza tengeneza compyuta kutoka ilivyo sambazwa hadi kukamilika kiasi cha kufanya kazi huku ukiwa na ujuzi kidogo wa jinsi ya kufanya assembling ya compyuta yaani kuunganisha vifaa vya computer hadi ikamilike compyuta inayo weza kufanya kazi.
Vifaa hivyo kama vile motherboard, cpu , video card, hard disk ,keyboard n.k
Ukisha maliza kuunganisha vifaa ili iwe uwe mfumo wa computer ambao vitu vyote au vifaa vyote ulivyo unganisha vinafanya kazi Pamoja na kutengeneza muungano wa kutatua tatizo flani.
Kiundani vifaa ulivyo tumia kuunda computer vinaweza kuwa mchanganyiko ambao umeundwa kwa namna mbalimbali na kampuni zaidi ya moja kwa njia na mitindo tofauti.
Pamoja na kufanikisha suala la kuunda hautakiwi au sio lazima kufahamu kwa undani mchakato wa kifaa kimoja kwamba kinafanyaje kazi kwa mfano ….. sasa CPU inafanyaje fanyaje kazi na inatumia umeme kiasi gani katika kufanya kazi yake ??? .
Taaluma yako inaishia kwenye kufahamu mwingiliano wa model mbalimbali za vifaa ili vifanye kazi bila shida yoyote yaani kwamba cpu haiwezi kufanya kazi kwenye system hii na hii inaendana na system.
Na ukisha fahamu mwingiliano kati ya vifaa hivyo. Basi kufanikisha zoezi la kuunda computer lina kuwa lahisi sana hata ikiwa imesambazwa vifaa vyake.
…………. Mwisho wa mfano………………….
Sasa hii inaingilianaje na programming .
OOP inatekelezwa kwa namna kama hii yaani kuunganisha tuvitu (vifaa) tunato fanya kazi tofauti tofauti ili kutengeneza kifaa(kitu).
ZINGATIA
Kuunganisha vitu vitu ili kutengeneza kitu.
Kwa kutumia OOP basi program yako inakuwa inaundwa na kama vifaa vinavyo jitosheleza yaani (objects) na kila object inakuwa na kazi yake katika program na zote object hizo zinakuwa na uwezo wa kuwasiliana kwa namna iliyo andaliwa.
Mengineyo:
Kitu kinaundwa na vitu vitu vingi kama vile mtu anaundwa na viungo vingi . Gari nalo linaundwa na vifaa vingi , So programming ni kazi ya kutengeneza vitu vitu ili kutengeneza KITU chenye kufanya kazi kusudiwa.
Kwa hiyo mfumo wa kutambua kwamba nataka kutengeneza kitu flani , kitu hicho kifanye kazi flani na ili kifanye kazi kina takiwa kiwe na vitu vitu flani. Ndio hiyo tunaita PROGRAMMING .
Yaani mfano nataka nitengeneze mfano wa BENKI basi ujue benki inafanya kazi gani may be kukopesha. Kwa hiyo lazima utengeneze kitu cha kukopesha katika benki yako hiyo.
MUHIMU
Wazo moja la project linaweza tekelezwa na programming language yoyote ile ama Java, python , C , C++ n.k
Baada ya kuchagua lugha ya kompyuta ambayo uko na uzoefu nayo , mchakato wa kwanza ni kuwaza mtililiko wa maelezo ambayo program ifanye (algorithms).
Pili ni kutengeneza maelezo (instruction au program) na kuwasilisha program hiyo kwa umma kwa namna ambayo wewe uko vizuri na inaendana na programming language ambayo umeitumia.
Mfano kama ni java unaweza kuwasilisha kwa namna yoyote kati ya hizi.
1. Web Application
2. Desktop Application
3. Mobile Application
4. Embedded kwenye mifumo ya hardware kama vile mashine za kufulia , printer n.k AU automation mshine mbalimbali za viwandani au printers , mashine za kufulia n.k
Kwa hiyo katika hizo utachagua namna ambayo ni rahisi kutokana na uzoefu wako ulio upata mahali popote.
Katika mfunzo ndani ya JIKU TECH TIPS tutajifunza kuwasilisha Mawazo yetu ya programs kwa namna mbili
- Web development na HTML, PHP na MYSQL.
- Mobile Application XML, JAVA, PHP, MYSQL.
Web development
Tutajifunza namna nzima ya kufanya web development kutoka mwanzo mpaka mwisho kwa silabasi iliyo andaliwa na JIKU TECH TIPS.
Mobile Application Development
Tutajifunza namna mzima ya kufanya web development kutoka mwanzo mpaka mwisho
Mafunzo na maelezo yanafanyika kwa njia mbili.
- Youtube video free
- eBook Paid
WEB DEVELOPMENT
tayari imekamilika ikiwa na video 8 na kitabu ambacho kimesheheni picha na maelezo yanayo elekeza vizuri .
Pamoja na hayo ili kuelewa vizuri katika suala hili na kupata ujuzi ulio kamilifu usiishie kuangalia video hizo nane huko youtube ni vizuri ukapata kitabu kwa gharama ya TSH 15, 000/= .
MOBILE APP PROGRAMMING
Imekamilika katika silabasi na kitabu chake rasmi kwa ajili ya mapito yanayo husiana na ujuzi wa jumla wa Android Programming, Kuna video zipo Youtube lakini utapata ugumu sana kuendelea na mafunzo hayo bila kuwa na mwongozo wa yapi ya kuzingatia na yapi ya ziada katika safari hii kulingana na nia yako.
Gharama ya kitabu cha Android Programming ni Tsh 10, 000/=
UTARATIBU WA KUPATA VITABU
Mara baada ya kufanya malipo kupitia namba 0682329852 ambayo ina jina ALEX ANOD NCHINGA kitabu unakipata kwenye WhatsApp yako muda huo huo baada ya malipo kuthibitishwa.
0 Comments