ELEWA KUHUSU TAALUMA AU UJUZI WA PROGRAMMING
Programming ni nini??
Kama una uelewa na TEHAMA endelea kuhusiana na programming
Programming ni kitendo cha kuandika maelezo au kuunda maelekezo au kuunda maelekezo kwa kutumia lugha flani ya kompyuta kwa ajili ya kufanikisha malengo flani
Mafanikio ya mtu anayefanya programming huwa ni kufanya development ya programu ya compyuta.
Unaweza ukajifunza taaluma hii mwenyewe kwa kutumia vyanzo mbalimbali lakini inapendekezwa ili kujifunza kwa haraka kidogo inakuwa inatakiwa sana mtu awe na mwalimu , na kwa nini mwalimu kwa sababu katika kujifunza taaluma hii ni ngumu kidogo kupata uhakika wa usahihi wa kile unacho kuwa unajifunza.
Hatua 6 za kufuata ili kubobea lugha flani ya computer
Siyo kama mwalimu yeye anakuwa anajua sana kile anacho kuelekeza hapana kile anacho kuambia mwelekezi wako ni kitu ambacho ukikipitia kwa mapana yake kutokana na uwezo wako wa kupambanua mambo unaweza kuwa bora kumzidi huyo mwalimu .
Mtu anayejifunza programming hupata uwezo wa kutatua matatizo kwa namna mpya na kuboresha uwezo wake wa ubunifu na ufanisi kwenye maisha yake.
Mtu anaye jifunza kompyuta programming yeye ankuwa na uwezo mkubwa sana wa kuelewa mifumo ya kompyuta na pia anachangia katika kuleta suluhisho flani mpya kwenye masuala mbalimbali ya teknolojia.
Kupitia kujifunza programming, mtu hupata uwezo wa kubadilisha mawazo kuwa vitendo vinavyotumika kwenye teknolojia.
Uwezo huu huleta fursa za kifedha na kazi mpya zenye mafanikio.
Pia programming inamwezesha mtu kushiriki katika miradi mingi ya ubunifu na kusaidia kutatua changamoto za kisasa kwa njia ya kidijitali.
Hatua 6 za kufuata ili kubobea lugha flani ya computer
Nita kuelezea kisa kimoja hapa kinacho nihusu mimi moja kwa moja.
KISA KILICHONIPA KUJIAMINI KATIKA PROGRAMMING
Mimi siku moja nilikaa na bwana mmoja sasa tukawa tunaongelea maisha na shughuli zetu za kila siku kila mtu kwa upande wake.
Sasa mimi nikawa naeleza sana shughuli zangu za programming jinsi nnavyo zifanya na zinafanyikaje.
Nikawa nimemwambia haswa tuna tabia ya kuskiliza sana matatizo ya watu hasa yale ambayo kuya rudia rudia yana mpa mtu wakati mgumu na hasa kuchosha sana, tunageuza changamoto kama hizo kwa namna inayoweza kuwa rahisi.
Bwana huyo akawa ananiambia kwa upande wake huwa na changamoto ya kutembea na notibuku (notebook) kwa ajili ya kuandika mienendo yake ya kazi kama vile matumizi, Tarehe aliyosaini mkataba wa kazi flani, Tarehe aliyo lipwa kiasi flani kwenye mkataba flani, akanieleza mambo kibao
Sasa mwisho kabisa akaniambia zikipita siku kadhaa taarifa hizo zote anazipeleka kwenye EXCEL ili kutunza kumbukumbu za mahesabu.
Hatua 6 za kufuata ili kubobea lugha flani ya computer
Nikawa nime muuliza , kwahiyo sasa hii ni sababu ya wewe kutembea na begi la kompyuta mara kwa mara kwenye begi lako , akanijibu Ndio.
Akaniambia afadhali tume ongelea haya leo , je tunaweza fanya kitu kurahisisha haya , Mimi nikasema Bila shaka.
Nikachukua fursa hiyo nikampa uzoefu wangu wa namna inayo wezekana kumsaidia kurahisisha michakato hiyo akiwa na simu yake.
Nakuwepo uwezekano wa kupakua EXCEL ambayo tayari inakuwa imeandaliwa kwa namna atakavyo yeye kila baada ya muda atakao yeye.
Na hii ndio taaluma ya programming, yaani kurahisisha mambo yanayo wezekana kurahisishwa kama ilivyo maana ya Teknolojia.
Kitu kinacho weza kuongezeka hapa kingine ni kwamba ujuzi wa programming huchangia katika kuboresha ustadi wa kimantiki,uwezo wa kufikiri ki mfumo, na uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka na sahihi.
Hivyo kujifunza programming ni muhimu sana katika dunia ya leo yenye teknolojia inayo badilika kwa kasi.
MASWALI MAKUBWA ANAYO JIULIZA MTU ANAYETAMANI KUJIFUNZA PROGRAMMING NA MAJIBU YAKE YA KIMTAZAMO.
Hatua 6 za kufuata ili kubobea lugha flani ya computer
Swali
Ninaanza kujifunza programming, je, ni lugha gani ya programming ninayo paswa kuanza nayo??
Jibu
Kwa wengi, Python ni chaguo zuri la kuanza kutokana na urahisi wa kujifunza na matumizi yake katika uwanja mpana wa teknolojia.
-------------------------------------
Swali
Ni chanzo kipi bora cha kujifunza programming kwa mazingira ya kujisomea??
Jibu
Mtandao una chaguo nyingi kama vile kozi za mtandaoni, vitabu na video zinazoelekeza kwa ujuzi wa awali hadi wa juu katika programming.
--------------------------------------------------
Swali
Je,ni lazima kuwa na shahada au mafunzo rasmi ya programming ili kufanikiwa kama DEVELOPER??
Jibu
Hakuna sharti la kuwa na shahada au mafunzo rasmi japo yanasaidia sana kuboresha uelewa wako . Ufahamu wa vitu vya msingi na mazoezi ni muhimu zaidi.
------------------------------------------------
Swali
Ni jinsi gani naweza kutatua changamoto na matatizo ninayo jaribu kupeleka taaluma yangu ya programming??
Jibu
Kujenga au kutatua changamoto ni sehemu muhimu ya mchakato wa kujifinza programming, labda kwa kuchimba zaidi kuwa na utaratibu wa kuuliza maswali na kujaribu suluhu au suluhisho tofauti tofauti kwa namna hii mtu unaweza kujifunza kutatua matatizo yanayojitokeza kwa kutumia programming.
-----------------------------------------------------------
Swali
Je,ni vip naweza kuboresha na kujenga jina langu (kufahamika) au kutengeneza namna inayoeleweka kama programmer????
Jibu
Fanya mazoezi kwa kufanya miradi(projects) mbalimbali , shiriki kwenye platform mbalimbali fuatilia fursa mbalimbali na endelea kukua na kishirikiana na watu wengine wanaofanya kazi katika taaluma kama yako yaani programming.
0 Comments