NINI
MAANA YA NICHE NA JINSI YA KUTENGENEZA
Niche ni kategoria inayolengwa kutangaziwa jambo flani hasa
kategoria hii huwa inalengwa sana na matangazo ya biashara .
Sio biashara tu, niche pia huzingatiwa na watu wanao taka
kujenga umaarufu flani kwa kundi flani la watu.
Ninapo sema kundi ninaweza nikawa nimekuchanganya kidogo
lakini kikundi katika nadharia hii namaanisha hadhira.
Wafanyabiashara wakubwa au wenye ujuzi wa kutangaza bidhaa
zao hutengeneza bidhaa wakilenga kuzitangaza kwa hadhira ya aina flani ambayo
ndio kwa utafiti wao hadhira hiyo changamoto zake zinahusiana namna flani na
bidhaa hiyo.
Hadhira hiyo huwa ni ndogo ,maalumu na ambayo imefafanuliwa
vizuri .
Ili kufanya masoko katika niche makampuni au mashirika
lazima watambue niche waliopo kwanza.
Masoko kwenye niche maana yake ni kuchuja hadhira kutoka
kwenye soko ambayo mahitaji yao ni ya pekee sana.
Kwa mfano mzuri makeup ni sector pana lakini katika soko
lake kuna makeup kwa ajili ya matatizo ya Ngozi , makeup kwa ajili ya wasanii
mashuhuli na mengineyo
Kwa mfano mkoa mmoja unaweza kuwa na watu zaidi ya milioni
moja lakini katika hao watu kuna Watoto ,vijana,watu wazima na wazee. Idadi yetu ni 1milioni lakini kuna
mchanganyiko wa watu hao , tufanye kama unabidhaa yako.
Basi katika hilo unaweza ukalenga kundi flani la watu kwa
kufuata elimu ya niche ambayo ili ulenge kundi flani la watu lazima utambue
kwanza bidhaa yako iko kwenye niche gani.
Mfano
1.
Michezo
2.
Afya
3.
Malazi
4.
Burudani
5.
Usafilishaji
6.
Mitindo
n.k
Mada yetu ni niche sasa unataka utangaze bidhaa yako katika
mkoa umesha fahamu kwamba bidhaa yako ni ya michezo moja kwa moja ukitangaza
bidhaa yako kiholela utaingia gharama ambayo haina maana yoyote kwa
kuwatangazia au kupoteza muda kwa kuwatangazia watu ambao hawahusiki kabisa na
bidhaa hiyo.
Mtu ambaye anaelewa Habari ya niche katika kutekeleza hili
ataandaa mkakati, kwa mfano anaweza aka lenga kwanza watu ambao wanapenda
michezo nitawapata katika matukio yapi au katika maeneo gani ili kutangaza
bidhaa yake kwa ufanisi na kupata faida.
Unaweza uka pata hadhira inayo penda michezo kwa ajili ya
kuitangazia bidhaa yako moja kwa moja lakini kuna kipengele cha umri pia , Je bidhaa yako ipo ki umri umri au ni kwa
yeyote anae pendelea michezo ??
Ikiwa labda bidhaa yako ipo inalenga Watoto lazima swali
lingine litaongezeka hapa kwamba ni wapi nita wapata Watoto wanao penda michezo
??
Kwanini
sasa tunakuwa tunazungumzia Habari ya niche ???
ukweli ni kwamba mtu anae zingatia suala la pesa
anauwezekano wa kupata mafanikio makubwa na faida kubwa katika jambo lake na
likawa la kudumu kwa urahisi. Ni uhalisia kwamba katika hadhira watu milioni kuna mchanganyiko wa
watu wanao pendelea kategoria mbalimbali na maanisha mitindo wengine michezo
wengine burudani ya muziki n.k
ukichukua uamuzi wa kutangaza bidhaa yako kwa idadi ya watu
hao ambayo inaonekana ni kubwa kuna
uwezekano mkubwa sana ukapata watu 3 au 2 kwa kila watu 100 kutoka kwa hao
1,000,000 kwa sababu wengine matangazo na bidhaa yako au jambo lako itakuwa ni
kama kelo kwao.
Lakini kwa yule ambaye atachukua uamuzi wa kuchakata soko hilo la watu 1 milioni moja na akachuja akapata labda watu 100,000 pekee labda ndio watu wa michezo basi kuna uwekano wa yeye kupata matokeo yenye mafanikio mfano kwa watu 100 anaweza uza hata kwa watu 20 na hao wanao baki sio kama hawajataka ni kwasababu tu za kibinadamu ndio zimewafanya wasinunue kwa muda huo na pengine kwa wakati mwingine wakawa na asilimia nyingi sana za kununua bidhaa yako kwa sababu wanafuraha kusikia mambo ambayo yanayapendelea.
Mala hii haija ishia hapa imeandikwa kwa upana katika kitabu chenye jina "NICHE + FOLLOWERS = PESA" kitabu kinauzwa kwa bei ya Tsh 5000/=
Kupata Pdf Fupi Fupi kwenye Whatspp
Weka taarifa za mwasilano katika fomu hii
0 Comments